Monday, 13 October 2014



Adabu ishike mkondo wake! Njemba aliyetajwa kwa jina moja la Jose amejikuta akichezea kichapo ‘hevi’ kilichomsababishia kuvunjika pua kwa tuhuma ya ukuwadi wa mke wa mtu, Ijumaa Wikienda lilikuwepo eneo la tukio.
Njemba aliyetajwa kwa jina moja la Jose akivuja damu baada ya kipigo.
Msala huo wa aina yake ambao ulivuta umati mkubwa ulijiri wikiendi iliyopita maeneo ya Makumbusho jijini Dar baada ya kijana huyo kuwekewa mtego na kukutwa na mke wa mtu akimsomesha.
Kijana Jose akiondolewa eneo la tukio asije kuumizwa zaidi.
Kwa mujibu wa jamaa waliomwekea mtego Jose (wa kwanza kulia pichani juu), jamaa huyo amekuwa sugu mtaani hapo kiasi cha kuwakera baadhi ya vijana wenye wapenzi na wake zao.Jose alishuhudiwa akila kichapo kutoka kwa vijana wasiotaka kufuata sheria bila shurti hadi akatiririkwa damu chapachapa puani baada ya kuvunjika pua.
Baadhi ya vijana bado wakiwa na gadhabu wakati wa kuamulizia ugomvi huo.
“Haiwezekani awe anawakuwadia wake zetu kwa wanaume wengine, leo tulipanga tumtoboe hata jicho moja ili liwe fundisho kwake na wengine wenye tabia kama za Jose,” alisema mmoja wa vijana waliokuwa wakimsulubu jamaa huyo.Vijana waliokuwa eneo la tukio wakizozana katika songombingo hilo.
Akizungumza na Ijumaa Wikienda, mwanaume aliyemwekea mtego Jose ambaye aliomba hifadhi ya jina gazetini alisema kwamba, waliamua kumpa mkong’oto kijana huyo baada ya kuchoshwa na vitendo vyake hivyo.
Baadhi ya vijana wenye hasira waliochoshwa na tabia ya kikuwadi ya Jose.
Alisema hata mkewe alishamuonya juu ya mazoea na Jose na kumweleza kuwa akimkuta tu na kijana huyo lazima atampa talaka jambo ambalo lipo kwenye ‘prosesi’.
Kwa upande wake Jose alishindwa kusema lolote huku akisikilizia maumivu ya kipigo hadi alipoondolewa eneo la tukio na wasamaria wema.

0 comments:

Post a Comment

Design by GG greggy| Blogger Theme by greggy - Premium Blogger Templates | NewBloggerThemes.com