Thursday, 4 December 2014

Ndege aina ya helicopter ya jeshi la Kenya
Ndege ya jeshi la KDF nchini Kenya imeanguka katika eneo la Kismayu nchini Somali.
Ndege hiyo ilianguka siku ya Alhamisi mwendo wa saa tisa na robo ilipokuwa ikirudi Kenya baada ya kutekeleza mashambulizi katika eneo la Jamaame kusini mwa Somalia.
Kulingana na msemaji wa Jeshi kanali david Obonyo: ''Ndege ya KDF iliokuwa ikirudi nchini Kenya baada ya kufanya mashambulizi katika eneo la Jamaame kusini mwa Somali,ilikumbwa na matatizo ya kiufundi na kuanguka katika eneo la Kismayu .
Kanali Obonyo hata hivyo hakusema iwapo kulikuwa na majeruhi yoyote.
Jeshi la Kenya limesema kuwa ndege hiyo ilianguka kutokana na hitilafu za kimitambo baada ya kufanya oparesheni katika eneo la Jamaane Kusini mwa Somalia.
Hata hivyo baadhi ya mitandaoa iliyohusishwa na kundi la AL shabaab imechapisha habari kuwa AL shabaab wamedai kuwa ndio waliodungua ndege hiyo mwendo wa saa tisa Alasiri, Afrika Mashariki.
Msemaji wa kiksoi cha kivita cha Al shabaab Sheikh Abdi Azizi Abu Musab amenukuliwa akisema kuwa walishambulia ndege hiyo kwa kombora baada ya kulipua kijiji cha Bulaguduud.
Kwa mujibu wa mwandishi wa BBC wa idhaa ya kisomali, ni vigumu kwa Al Shabaab kufanya shambulio kama hilo katika mji wa Kismayu kwa kuwa eneo hilo zima limefurika vikosi vya usalama vya AMISOM.
Mnamo mwaka wa 2012, majeshi ya Kenya yaliuteka mji wa bandari wa Kismayu, unaotazamiwa kuwa mji muhimu sana wa kiuchumi katika eneo zima la Somalia kutoka kwa wanamgombo hao wa Al shabaab.

 0
Hili ni basi ambalo limetumbukia shimoni kwenye mlima Kitonga mkoani Iringa.


Basi lililotumbukia shimoni bila abiria lilikuwa likivutwa, na haikuwezekana. Njia ilifungwa na mamia ya wasafiri tulibaki eneo la tukio kwa saa mbili na nusu.VICTOR SIMON


Idadi ya watu waliokufa kutokana na ajali ya moto wa lori lililopinduka na kisha kulipuka baada ya watu kulivamia kwa lengo la kujipatia mafuta, imeongezeka na kufikia watano kutoka vitatu vya awali.
Hayo yamethibitishwa na Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova.
Alisema katika ajali hiyo iliyotokea juzi usiku eneo la Mbagala, watu 16 walijeruhiwa baada ya kuungua maeneo mbalimbali ya miili yao.
Ajali hiyo ilihusisha lori aina ya Scania lenye namba za usajili T 347 BXG mali ya Moil Transporter lililokuwa likitarajiwa kusafirisha mafuta kuelekea Kampala, Uganda likiwa na kemikali aina ya petroli lita 38,000 inayokadiriwa kuwa na thamani ya dola 36,000 (Sh milioni 60).
Aliwataja waliokufa kuwa ni Hassan Mohammed (25), mkazi wa Mbagala Kimbangulile, Masoud Masoud (33), Mohammed Ismail (19), Ramadhani Khalfan (36) na Maulid Rajabu, wakazi wa Mbagala Charambe.
Majeruhi waliotambuliwa ni Hamis Ally (35), mkazi wa Mbagala Kiburugwa, Rajabu Selemani (28), mkazi wa Tandika, Idd Said (28), Janney Mathayo (25), mkazi wa Mbagala Kizuiani, Mathayo Daniel (21), mkazi wa Mbagala Charambe na askari polisi, Koplo Thomas aliyejeruhiwa na jiwe kwenye paji la uso wakati akijaribu kuzuia vibaka kuchota mafuta kabla ya kulipuka.
Alisema majeruhi wengine 10 wamelazwa katika hospitali ya Taifa Muhimbili na Hospitali ya Wilaya ya Temeke wakiendelea na matibabu na wengi wao hali zao siyo za kuridhisha.
Kamanda Kova aliongeza kuwa, mbali ya kusababisha vifo na majeruhi, ajali hiyo pia ilisababisha kuungua kwa nyumba ya kulala wageni iitwayo United yenye vyumba 32, mali ya Deus Kasigwa (42), mkazi wa Mtoni Mtongani. Moto huo uliteketeza pia maduka matano yenye vitu vyenye thamani ya Sh milioni 197 na pipikipiki saba ziliteketea kabisa na moto.
Naye Ofisa Uhusiano wa Hospitali ya taifa ya Muhimbili, Doris Ishenda alisema majeruhi 11 wanaoendelea kutibiwa hospitalini hapo, huku akiongeza kuwa, hali zao sio nzuri kwa kuwa waliunguzwa vibaya na moto na kwamba madaktari wanaendelea kuwapatia matibabu.
‘’Majeruhi wote wamelazwa katika wadi namba 22 ya Sewa Haji wanaendelea na matibabu, lakini hali zao sio nzuri kabisa kwani waliungua sana,’’ alisema Ishenda.
Wakati huo huo, Paulo Milanzi (35), mkazi wa Chanika katika manispaa ya Ilala anayetuhumiwa kushiriki katika mauaji ya Ofisa Usalama wa Taifa, Sylvanus Mzeru, amefariki dunia baada ya kupigwa risasi katika majibizano na polisi.
Kova alisema mtuhumiwa huyo alikuwa akitafutwa na polisi kwa muda mrefu kuhusu matukio mbalimbali ya mauaji na unyang’anyi wa kutumia silaha jijini Dar es Salaam na mikoa ya jirani.
Hili ni basi ambalo limetumbukia shimoni kwenye mlima Kitonga mkoani Iringa.


Basi lililotumbukia shimoni bila abiria lilikuwa likivutwa, na haikuwezekana. Njia ilifungwa na mamia ya wasafiri tulibaki eneo la tukio kwa saa mbili na nusu.VICTOR SIMON

Katika Gazeti Pendwa la Ijumaa toleo namba 679 lilinasa picha za mwanama mmoja ambaye jina lake lilidaiwa kuwa ni Tuma ambaye inasemekana kuwa ni mtoto wa kigogo akiwa amepiga picha chafu na njemba moja ambaye hakujulikana anafanya kazi wapi, sasa majibu yamepatikana.


 Habari za kiuchunguzi za gazeti hili zimebaini kuwa jamaa huyo aliyekuwa na mrembo huyo kumbe anaitwa Kamau Isaack na ni dereva katika Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto.

Habari hizo zinadai kuwa watu hao walifotoa picha hizo mbaya za kimahaba wakiwa mjini Tanga na hivi sasa zimesambaa jijini Dar es Salaam.

Ilidaiwa kuwa, mara kwa mara mwanaume huyo alikuwa akimuaga mkewe kuwa anasafiri kikazi kumbe alikuwa akiishia kuponda raha na Tuma.

Aidha, imeelezwa kuwa mwanadada huyo sasa anajuta na anahaha kwa kuwa alikuwa akiiba mume wa mtu.

“Unajua huyu jamaa ameajiriwa katika wizara ya mama Sitta ni dereva na amekuwa akisafiri mara kwa mara, lakini haijajulikana kwanini walipiga picha hizi mbaya, ambazo ni kinyume cha maadili,” kilisema chanzo chetu.

Katika uchunguzi uliofanywa na gazeti hili imebainika kuwa mume huyo wa mtu amekuwa si mkaaji sana wa nyumbani kutokana na majukumu mazito ya kikazi yanayomfanya awe safarini mara kwa mara.

Gazeti hili bado linaendelea kufanyia uchunguzi picha zingine ambazo zinatajwa kuwa ni chafu zaidi ambazo haziendani na maadili ya Kitanzania zilizotapakaa mitaani.
 Awali, Kamau alipopigiwa simu na kuulizwa kuhusiana na picha hizo alizikana huku Tuma akisakwa kwa udi na uvumba kupitia simu yake ya mkononi bila mafanikio
Stori: Erick Evarist na Imelda Mtema
NYOTA wa Nyimbo za Injili Bongo, Rose Mhando (pichani)amefungukia eneo fupi la maisha yake magumu ambapo alisema amewahi kutekwa kwa bastola na mwanaume mmoja, akampeleka msituni ambako alimlazimisha kuwa naye kimapenzi lakini akadunda.Akizungumza na Gazeti la Amani juzi, Rose alieleza kwa machungu kwamba, tukio hilo lilimkuta hivi karibuni mjini Dodoma ambako ndiko kwenye makazi yake ya kudumu.Ilikuwa ni katika mahojiano ya kukiri kwake (my confession) ambapo Rose aliweka bayana kuhusu mazingira ya tukio hilo la kushangaza.

MSIKIE MWENYEWE
“Dunia ina mambo mengi sana ndugu zanguni, wengine wema, wengine waovu. Mimi nakumbuka siku moja kuna mwanaume ambaye nilikuwa na ukaribu naye.“Huyu bwana, ana jina kubwa sana Dodoma. Alinichukua kwenye gari kwa ajili ya kunisaidia mambo fulani maana alikuwa ananisaidia katika kazi zangu.
“Nilishangaa kumuona anapeleka gari nje ya mji,  nikamuuliza tunakwenda wapi, akasema tulia utajua.
“Sikuwa nimemuwazia ubaya, hivyo nilitulia lakini matokeo yake akanipeleka hadi porini ambako alikutana na watu wengine, naamini walikuwa wasaidizi wake.
“Naamini ulikuwa mpango kabambe. Wale watu wakaniweka chini ya ulinzi na kunifunga kamba kisha wakanioneshea mtutu wa bastola,” alisema Rose huku akisisitiza ni tukio ambalo hawezi kulisahau.
AAMBIWA KISA
Rose aliendelea kudai kuwa, mpaka hapo hakuwa amejua kisa lakini akiwa amekutana macho na mdomo wa bastola. Ndipo akaambiwa kuwa, anatakiwa kuwa chini ya himaya ya kimapenzi ya mwanaume huyo la sivyo siku zake zilikuwa zinahesabika.“Niliona ni jambo la ajabu, kwani mwanaume kumtaka mwanamke ni mpaka silaha na kutishia kuua?” alihoji staa huyo mkubwa wa gospo.
AKUBALI YAISHE
Rose aliendelea: “Kwa pale nilikubali kwamba niko tayari kuwa mtu wake lakini nikamwambia tukirudi mjini tukae tuongee kwa kirefu, akakubali.“Tulifika mjini nikiwa najisikia kuumwa sana maana wale wasaizidi wake walikuwa wakinisulubu kwa kunipigapiga pia ile kamba niliyofungwa ilichangia kunipa maumivu makali.”AKACHA KUKUTANA
Rose alisema walipofika mjini walipanga kukutana baadaye ili wayaongee lakini yeye akakacha kutokea kwenye kikao, hivyo akaenda polisi (hakutaja kituo) ambako alifungua jalada la uchunguzi.“Nimekuwa nikisita kumwanika kwa jina huyo mwanaume kwani yupo na ni adui yangu mkubwa. Naishi kwa tahadhari kubwa sana, naamini siku nikimtaja ataniua.
“Mbaya zaidi najua mambo yake mengi, mabaya kwa mazuri lakini mabaya ni mengi sana kwani hata wakati ananisaidia kuhusu kazi zangu alinitenda maovu mengi, nimemwachia Mungu.”
KWA NINI AMEAMUA KUSEMA?
“Nimeamua kusema ili moyo wangu uwe mweupe, nimekuwa nikiwaza siku hadi siku kuhusu lile tukio, ni kumbukumbu mbaya sana kwangu, lakini kwa kukiri kwangu huku sasa nitakuwa na amani.”
Amani: “Polisi walichukua uamuzi gani?”
Rose: “Walisema wanafanya uchunguzi wa kina lakini sijawahi kuambiwa walifikia wapi!”
Amani: “Baada ya kuingia mitini jamaa hajawahi kukutumia meseji ya kukutishia maisha?”
Rose: “Hapana, alijua nimekwenda polisi.”


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, David Misime.
Amani: “Unadhani ni kwa nini alikuteka hadi msituni, kwa nini asikwambie tu kawaida mjini?”
Rose: “Alishawahi kuanza hizo dalili za kunitaka nikamwonesha sitaki, nilimwambia nataka kazi kwake na si mapenzi. Mimi najua fedha ndiyo jeuri yake.”                    
Amani: “Ana familia?”
Rose: “Ana mke na watoto.”
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, David Misime alipotafutwa hakuweza kupatikana kuzungumzia ishu hiyo.

ULEVI noma! Ndivyo unavyoweza kusema kuhusu kilichomtokea mtoto wa kigogo mmoja aishie Masaki ambaye alijikuta akifanyiwa kitu mbaya ndani ya maji kwenye ufukwe wa Bahari ya Hindi, eneo la Coco jijini Dar, Jumamosi iliyopita. 



Binti akijiachia na njemba huyo baada ya kupiga urabu wa kutosha.Kabla ya tukio hilo, inadaiwa kuwa dada huyo ambaye jina lake halikuweza kufahamika mara moja, alikesha katika klabu moja iliyopo ufukweni hapo, akipiga ulabu yeye pamoja na kampani yake.Ilipofika asubuhi, inadaiwa kuwa, ili kupunguza ulevi aliokuwa nao kichwani, aliamua kwenda kuogelea, ili akae sawa.
Chanzo kilichoshuhudia tukio hilo kilishadadia maneno kwa mpigapicha wetu kwa kusema kuwa, wakati mrembo huyo anaenda kuogelea ndipo alipoangukia kwenye mikono ya njemba mmoja aliyekuwa akifanya mazoezi pembeni mwa ufukwe huo ambapo pia alikutana na wachezaji wa Azam FC waliokuwa wakifanya mazoezi mambo yakaharibika.


...Akionyesha kufurahia hali hiyo.“Wakati anawafuata wale wachezaji, redio za watu wa bajaj zilikuwa zimefungulia muziki kwa sauti, akawa anacheza, jamaa walipoona vile wakaongeza sauti na kumwekea wimbo wa Davido wa Aye, dah, ndio akachizika kabisa, jinsi alivyokuwa akikata mauno na nguo alizovaa, aliwachanganya kabisa wachezaji wa Azam ambao walikuwa wakimtumbulia macho kwa udenda,” kilisema chanzo hicho.
Baada ya kuwapagawisha wachezaji hao, binti huyo alipomfuata njemba mmoja aliyekuwa kando na kumuomba amfundishe kuogelea, jamaa akachukua tairi la gari na kumwingiza baharini ambako alianza makeke ya kumfundisha huku wakizamia kuonesha kuna kamchezo kachafu kanaendelea.
 
Baadaye akiwa kama aliyeshtuka, alikurupuka majini humo na kutoka nje akikimbia, akimuacha njemba aliyekuwa naye baharini akimtumbulia macho ya kutoamini kilichotokea.
Misiba ya vijana wawili,Matei John Mmassy Mfanyabiashara na mmiliki wa Klabu maarufu mjini Dodoma ya Matei Lounge na Wakili wa kujitegemea na Mkufunzi wa Chuo Kikuu cha St. John, Joseph Joshua Oguda waliofariki kwa ajali ya gari maeneo ya Ranchi ya mifugo,Narco iliyopo Kongwa nje kidogo ya mji wa Dodoma mapema wiki hii wakitokea Mjini Morogoro vimetikisa mji wa Dodoma na Viunga vyake.

Miili ya marehemu hao imeagwa leo kuanzia mchana katika ibada ya pamoja iliyo fanyika katika Uwanja wa Nyerere Squire mjiji Dodoma.Miili yote imesafirishwa jioni hii wakati Mwili wa Marehemu Matei umepelekwa Mkoani Kilimanjaro na Mwili wa Marehemu Joshua Ogunda umepelekwa Musoma,Mkoani Mara kwa ajili ya tararibu za Mazishi.

Majeneza yenye miili ya marehemu Joshua na Matei wakati wa ibada maalum ya kuwaombea iliyofanyika kwenye Uwanja wa Nyerere mjini Dodoma

Sehemu ya Umati wa waombolezaji wa Misiba hiyo.


Waombolezaji wa wakiwa kwenye foleni ya kwenda kuaga miili ya Marehemu hao.

obama and malia

Now please take this information with a pinch of salt, a satire website dubbed Empire News claims that Barack Obama’s daughter, 16-year-old Malia, has confirmed that she is pregnant.
According to Empire news Malia is now in her second trimester and First Lady, Michelle Obama, says that although she will be a grandmother much younger than she planned, teen pregnancy runs in the family……apparently Obama’s mum had him at the age of 18.
The father of the ‘child’ is not known but he is white…..like that has helped in any way. Chances are that this is all a hoax and since we all have been entertained let life continue.
Design by GG greggy| Blogger Theme by greggy - Premium Blogger Templates | NewBloggerThemes.com