Wednesday 22 October 2014










Rais Jakaya Kikwete akiwapungia wafanyakazi wa Hoteli ya Diaoyutai ya mjini Beijing mara baada ya kuwasili nchini China kwa ziara ya kikazi.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amesema kuwa mfumo wa Tanzania ambako Rais anatumikia nafasi ya uongozi kwa muhula wa miaka mitano na siyo zaidi ya miaka 10 ni mfumo mzuri na unaovutia kwa sababu unaiwezesha nchi kupata fikra na mawazo mapya.Aidha, Rais Kikwete alisema kuwa anaamini Tanzania itapata Rais bora zaidi kuliko yeye, Rais ambaye ataiwezesha Tanzania kusonga mbele kwa kasi kubwa zaidi. Rais Kikwete pia alisema kuwa, anayo hamu kubwa ya kumaliza muda wake wa uongozi, ili arudi kijijini kushughulika na wajuu wake na mifugo yake.Rais Kikwete alitoa kauli hiyo Jumatano, Oktoba 22, 2014, mjini Beijing, China, wakati akizungumza na mabalozi wa Afrika wanaoziwakilisha nchi zao katika China.Mkutano huo uliofanyika kwenye Nyumba ya Kufikia Wageni wa Serikali ya China ya Diaoyutai, ulikuwa shughuli ya kwanza ya Rais Kikwete katika ziara yake rasmi ya siku sita ya Jamhuri ya Watu wa China ambako amealikwa na Rais Xi Jinping.Wakati wa maswali na majibu, Mheshimiwa Balozi Sola Onadipe, Naibu Balozi wa Nigeria katika China, alishangazwa na kauli ya Rais Kikwete kuwa anatamani amalize muda wake wa uongozi, ili astaafu na kusema kuwa lingekuwa jambo la maana kwa Afrika kama viongozi wengine wangekuwa na mawazo ya namna hiyo ya kuheshimu Katiba za nchi zao na kung’atuka kwenye uongozi muda wao unapowadia.Rais Kikwete alimwambia Balozi huyo: ” Ni kweli naona kama muda hauendi kwa kasi ya kutosha, ili niweze kuwa raia wa kawaida na nipate muda wa kuchunga ng’ombe na mbuzi wangu na nilime mananasi yangu kwa nafasi ya kutosha. Lakini Mheshimiwa Balozi usishangazwe na utayari wangu kuondoka katika uongozi.”“Kwanza utaratibu huu wa miaka mitano ama miaka 10 ni utaratibu wa Kikatiba, ni jambo lililoko katika Katiba yetu na hatuna kishawishi cha kulibadilisha. Pili, kazi hii ya Urais ni kazi ngumu sana. Kwa hakika, binafsi nawaonea gele sana wenye nguvu na ubavu wa kutaka kubakia kwenye kazi hii kwa miaka mingi. Pengine wana nguvu zaidi kuliko mimi,” amesema Rais Kikwete na kuongeza.“ Lakini pia kuna uzuri katika mfumo huu wa kwetu kwa sababu kila baada ya miaka mitano na hata kama ni baada ya kila miaka kumi, anaingia mtu mwingine madarakani akiwa na fikra mpya na mawazo mapya.”“ Mfumo huu ni mfumo unaoniridhisha sana na wala hakuna kinachonishawishi nibakie katika madaraka zaidi ya muda wangu kikatiba. Nina hakika, nchi yetu itapata kiongozi mwingine, bora kuliko hata mimi, kuongoza vizuri nchi yetu.”
Rais Kikwete pia amesema kuwa siyo busara pia kwa kiongozi kuwasikiliza wale wanaoshauri wakisema kuwa akiondoka madarakani nchi itavurugika.“Kwa hakika, hawa wanatetea maslahi yao tu wakisema kuwa ukiondoka wewe madarakani, wao hawatakuwa tena mabalozi ama mawaziri ama nafasi nyingine yoyote.”



 










Familia ya ndugu Aron Sondi inayeishi Kigamboni jijini Dar es Salaam, ambao taarifa zikiambatana na picha za kuungua kwa nyumba na kupoteza mali na vitu vyote jana jioni zimekuwa zikisambaa kwenye mitandao (zimepachikwa hapo chini), wanaomba michango ya hali na mali. 


Atakayeweza kusaidia kwa vyovyote tafadhali awasilishe michango kupitia namba ya Aron0763210530 au kupitia Tigo pesa ya mke wake, Sara Obel: 0713560844.




Mmoja wa waliomuangushia kichapo mwanamke huyo hadi akafariki
Kisa cha kushangaza kilitokea nchini Nigeria ambapo mwanamke mmoja alipewa kichapo cha mbwa hadi akafariki kwa madai ya yeye kuwa mchawi.
Mwanamke huyo inasemekana alikuwa Ndege iliyokuwa inaruka mtini kabla ya kugeuka na kuwa binadamu.
Umati wa watu ulikusanyika eneo alilokuwa mwanamke huyo baahi wakinasa matukio kwenye simu zao za mkononi. Polisi wawili walilazimika kurusha mabomu ya petroli kuwatawanya watu hao na kuwazuia kunasa picha za mwanamke huyo aliyekuwa anachapwa sana.
Kwa mujibu wa walioshuhudia, mmoja alisema kuwa mwanamke huyo dakika chache zilizopita alikuwa Ndege mtini kabla ya kugeuka na kuwa mwanamke.
Ndege huyo alikuwa anazunguka mti mjini Oshodi , kisha akagonga mlingoti wa stima kabla ya kuanguka ardhini ambapo aligeuka na kuwa mwanamke.
Hii ni kwa mujibu wa wakazi wa mjini Oshodi wanaodai kuwa mwanamke huyo alikuwa mchawi.
'Kitu cha kushangaza'
''Ni kitu cha kushangaza lakini ni cha kweli,'' alisema bwana Sobowale.
"tulipozungumza na mwanamke huyo alidai kuwa na nguvu za kiganga, na kwamba alikuwa amewaua watu kadhaa. Aliongeza kuwa alikuwa anarejea kwa mumewe anayeishi katika eneo la Mushin kabla ya tyukio hilo. Baadhi ya watu walianza kumpiga picha. ''
Video ya umati huo ukimtandika mwanamke huyo imeenea kama moto msituni na kutazamwa na maelfu ya watu kwenye mtandao wa kijamii wa YouTube.
Mwanamke huyo alikuwa uchi wa mnyama huku ngozi yake ikiwa inatoka baada ya kuchomwa.
Banke Idowu ni mmoja wa watu walionasa video ya mwanamke huyo akiwa anachapwa na umati na kwamba alikuwa amearifiwa na wenzake kuhusu mwanamke huyo alivyobadilika.
Aliambia BBC kuwa "sijawahi kuona jambo kama hili maishani mwangu,lakini nimesikia na kuona tu kwenye filamu kwa hivyo waliponiambia kuwa limetokea , mimi nimeamini. ''
Alisema angedhubutu kumuokoa mwanamke huyo umati huo ungemgeukia na yeye.
Polisi hawajuzungumzia tukio hilo, hususan kabla ya umati huo kukusanyika na kuanza kumchapa mwanamke huyo.
Alifariki mda mfupi baadaye huku mwili wake ukipelekwa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali kuu.

Koo mbili za Wanyazaga na Wambukwa mnyambwa wakiwa wamekusanyika kukizunguka kisima kinachosemekana kimejaa maajabu cha Bwibwi kilichopo Katika kijiji cha Iyumbu kilichopo pembezoni mwa Chuo kikuu cha Dodoma [UDOM]


Baadhi ya wananchi wakifurahia kutumia maji yanayopatikana kisima cha Bwibwi kilichopo katika kijiji cha iyumbu Manispaa ya Dodoma, kisima hicho kilichovumbuliwa katikati ya miaka 1,800 kiko katika hatihati ya kufukiwa na eneo hilo lituumike kwa matumizi mengine.


Mkuu wa kimila wa kabila la kigogo Lazaro Chihoma akinywa maji yaliyochotwa kisima cha Bwibwi kilichopo Kijiji cha Iyubu Manispaa ya Dodoma, Kisima hicho kinachoaminika ni cha maajabu na mtu anayetumia maji yake hupata Mafanikio ya kiafya na kimaisha:



Ni masaa machache tu yamepita tangu muziki wa kizazi kipya Tanzania, Bongo Fleva kumpoteza aliyekuwa staa wa muziki huo kutoka kundi la TMK Wanaume Family, aliyekuwa akifahamika kwa jina la YP, taarifa nyingine ya simanzi inahusu msiba wa aliyekuwa muigizaji wa Bongo Muvi.
Katika ukurasa wake wa instagram, muigizaji na mchekeshaji maarufu anayefahamika kwa jina la Kitale ama Mkude Simba (@mkudesimbaoriginal), amepost picha ya muigizajiShery Mwana aliyefariki masaa machache yaliyopita.
Kwa mujibu wa Kitale, muigizaji huyo mbaye jina lake halisi ni Sherry Charles Magali, aliwahi kushiriki na Kitale katika movie mbali mbali ikiwemo Kipotabo na Nyumba Nne.

Untitled33
Mfalme wa Kusini,Clifford Joseph Harris, Jr aka T.I baada ya kuacha historia kubwa Tanzania katika Tamasha la Serengeti Fiesta 2014 Oct 18 Leaders Club Dar es Salaam, Mkurungenzi Mtendaji wa Clouds Media Group,’Joseph Kusaga’ alimkabidhi msanii huyo zawadi  yenye mfano wa silaha za jadi.
.
.
Itazame  video hapa mtu wangu uone jinsi alivyokabidhiwa zawadi hiyo
Ni halali yako kupata kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza 

Marehemu Yesaya Ambikile Mwakalekamo  'YP' amezikwa hii leo katika makaburi ya Changombe jijini Dar es salaam.

Marehemu YP alifariki jana baada ya kuugua kifua na kulazwa katika Hospitali ya Temeke hadi mauti yalipo mkuta.

Awali kabla ya maziko hayo YP aliagwa na ndugu jamaa na marafiki zake katuika viwanja vya sigara Chang'ombe ambapo wasanii mbalimbali wa muziki wa Bongo fleva na Bongo muvi walihudhuria.
 
 YP kabla ya kuhamia katika sanaa ya uimbaji na kuibuka na kundi la wanaume Family alikuwa akifanya sanaa ya maigizo na vichekesho akiwa kundi moja na wasanii, Masanja Mkandamizaji, Mpigapicha maarufu na Blogger Mroki Mroki, Kiwewe, Dokii enzi hizo wakiwa na kundi la Get Well Generation lililokuwa chini ya Dokii na kurusha michezo yake Star Tv.

YP enzi za uhai wake aklitamba na nyimbo kama 'Ulipenda Pesa', 'Pumzika', 'Shemsha' na nyimbo nyingi za TMK Wanaume Family kama 'Twende zetu' ya Chege, 'Dar mpaka Moro', 'Kichwa kinauma', 'Tufurahi' na nyimbo nyingi za TMK Wanaume family pia alivuma na wimbo wa Binadamu Visa alioimba na swahiba wake, Y-Dash.


Kiongozi wa kundi la Yamoto Band na TMK, Mkubwa na Wanawe, Saidi Fela akizungumza wakati wa msiba huo. 























































Design by GG greggy| Blogger Theme by greggy - Premium Blogger Templates | NewBloggerThemes.com