Wednesday 22 October 2014

 Msanii wa HipHop kutoka Atlanta USA, callif Harris jnr au T.I alikuepo nchini kwa ajili ya Tamasha la Serengeti Fiesta na kuna vitu vichache ambavyo tunaweza kujifunza kutoka kwake, au tunaweza mtumia ili kukuza Soko la Music wa Tanzania. 
1.KUTOKUA NA UMIMI
Wakati anaperfom kwenye steji T.I aliimba hadi nyimbo za wasanii wengine wa America,kwanini wasanii wa Tanzania wasifanye hivi wanapopata nafasi ya kuperfom kwenye Matamasha makubwa nje nchi? je hii halitaweza kuwatambulisha wasanii wengine ambao hawajapata nafasi ya kujulikana nchi za nje? mimi naona iwapo wasanii watajifunza kitu hapo wanaweza kusaidia music wa Tanzania kukua zaidi. 

                                      T.I na crew take wakiwa wamevaa Mashati ya Asili kutoka Tanzania.
2.UBALOZI NA CALLABLE
   Pia Tulishuhudia T.I akiperfom ngoma ya Psqure "Ejajo" ambayo ameshirikishwa, sasa wasanii wa Tanzania wajiulize  T.I anafanya show nchi ngapi na hata kama T.I ataiimba hiyo ngoma kwenye show 3 kati ya show zake 10 Psquare watakuwa wapi baada ya Muda fulani? Nadhani Wasanii wa Tanzania ni muda wa kuwatumia wasanii wa nje wanaokuja kufanya Matamasha nchini, kwa mfano tunaweza angalia mafanikio aliyofikia Diamond baada ya kufanya collable na davido, sasa davido ni msanii kutoka Africa je ingekuwaje kama angefanya collable na Luda criss au RickRoss ambao wote wameshakuja Nchini.
3.PERFOMANCE
  Kama ulikuwa makini wakati wa show ya Fiesta utagungua kuwa T.I alikua anaperfom kama underground anayetafuta kutoka, Mbali na ukubwa wake katika Music,T.I hakudharau show, ofcourse T.I amewahi kufanya show kubwa zaidi ya Fiesta na wasanii wakubwa zaidi ya wasanii walioperfom kwenye Fiesta lakini T.I alifanya show ya nguvu sana, Tofauti na wasanii wengi wa Tanzania wanapopata nafasi kufanya show mikoani au show ndogo huwa wanadharau sana kiasi cha hata kutoipromote show hizo, Ukiangalia Page ya Instagram ya T.I na wall yake ya Twitter siku moja kabla ya show utagundua kitu, alikua akiipromote sana show ya Fiesta,kiasi cha mitandao mikubwa Duniani kuripoti kuhusu ujio wa T.I Tanzania na kuhusu show ya Serengeti Fiesta

0 comments:

Post a Comment

Design by GG greggy| Blogger Theme by greggy - Premium Blogger Templates | NewBloggerThemes.com