Thursday 15 January 2015

Stori: Joseph Ngilisho, ARUSHA/UWAZI  
MAZISHI ya Carista Charles Makoi, 52, (pichani), ambaye alikuwa mke wa mfanyabiashara bilionea jijini hapa, Charles Makoi yamefanyika huku shilingi milioni 200 zikisemekana kuteketea kwa bajeti. 

Mfanyabiashara maarufu jijini hapa, Patrick Ngiloi ambaye ni mmiliki wa vituo vya mafuta vya Kampuni ya Panone ndiye aliyekuwa mwenyekiti wa kamati ya mazishi hayo.
Baadhi ya wananchi wakishuhudia ajali iliyosababisha kifo cha Carista Charles Makoi.
 Kwa mujibu wa chanzo makini ndani ya kamati hiyo, siku ya kwanza tu baada ya kifo hicho, saa tatu mbele zilichangwa zaidi ya shilingi milioni 75 na baada ya hapo ziliendelea kuchangwa hadi kufikia lengo. 

WACHANGAJI WAKUBWA
Chanzo kilisema kuwa, wachangaji wakubwa walikuwa wafanyabiashara wakubwa kutoka mikoa ya kaskazini mwa Tanzania, ikiwemo Arusha, Kilimanjaro na Tanga.“Wengi waliowahi kuchanga ni wafanyabiashara wa mikoa hiyo niliyokutajia. Lakini tulidhamiria bajeti iwe ya milioni mia mbili. Unajua shughuli ni shughuli siku zote. 

“Tunaposema milioni mia mbili tulimaanisha kwa ajili ya kununulia vinywaji, kama bia, maji na soda. Pia vilinunuliwa vyakula mbalimbali, jeneza, sare na kuandaa mahali pa kukaa waombolezaji kutoka sehemu mbalimbali. Waombolezaji walikuwa wengi sana ndiyo maana bajeti ilikuwa kubwa.

“Kwa kweli tulikwenda sawasawa, hakuna mahali tulikwama. Ni bajeti ya aina yake hii,” kilisema chanzo hicho na kuomba hifadhi ya jina lake. 
 
...Wananchi wakiutoa mwili wa Carista Charles Makoi baada ya kubanwa kwenye gari.
 WALIVYOSEMA WAOMBOLEZAJI
Baadhi ya waombolezaji walisikika wakiteta kuwa, bajeti hiyo ilitosha kufanya miradi kadhaa ya maendeleo kama kununua madawati, vyandarua mahospitalini na magari kwenye vituo vya afya. 


“Mfano, nimesikia kwamba jeneza peke yake ni shilingi milioni saba, si unaweza kununua Toyota Vitz?” alihoji mwombolezaji mmoja na kujibiwa na mwenzake kwamba, mawazo kama hayo ni kuingilia uhuru wa familia ya marehemu.   Hii ndiyo ajali iliyoondoa uhai wa Carista Charles Makoi (52).
“Marehemu alikuwa na gari zaidi ya Vitz, unaposema inaweza kununua Vitz unamaanisha nani sasa? Wakupe wewe ukanunue au ndugu yako? Huko ni kuingilia uhuru wa familia ya marehemu,” alihoji mwombolezaji mwingine. 

MAZISHI YA AINA YAKE KIBOSHO
Baada ya msiba Arusha, msafara ulianza kuelekea Kibosho mkoani Kilimanjaro ambako marehemu alizikwa Ijumaa iliyopita nyumbani kwa familia hiyo, Sambani, Kibosho.Yalikuwa mazishi ya kwanza kwa idadi kubwa ya waombolezaji kutoka Arusha, Kilimanjaro, Tanga, Mwanza, Dar es Salaam, Morogoro huku magari ya kifahari yakiwa mengi.WAOMBOLEZAJI WALIACHA BIA
Wakati wa msiba huo uliokuwa maeneo ya Sakina jijini hapa, waombolezaji wanaopata ‘yale mambo’ walikunywa pombe mbalimbali zikiwemo bia na ilifika mahali walizikodolea macho kwa kinai kama si kulewa. 
“Da! Hii balaa, hapa mtu usipojiangalia unaumbuka hivihivi unajiona, mimi bia basi tena, sasa nakwenda na maji kwanza,” alisikika akisema mmoja wa waombolezaji msibani siku ya kwanza. 

MAKOI NI NANI?
Mume wa marehemu Carista, Charles Makoi anamiliki hoteli maarufu iliyopo jijini Arusha inayojulikana kwa jina la Aquiline (ghorofa 7), vituo vya mafuta Arusha na Moshi, maduka ya bidhaa mbalimbali jijini Dar, Morogoro, Kilimanjaro, Iringa na Tanga.
Anaishi kwenye nyumba kubwa ya kifahari iliyopo Sakina. 


TUJIKUMBUSHE
Marehemu Carista alipata ajali Januari 5, mwaka huu baada ya gari alilokuwa akiendesha kutoka Moshi kwenda Arusha, Mitsubishi Pajero lenye namba za usajili T 930 AVZ kugongana uso kwa uso na basi aina ya Hino (Mrindoko Trans) lenye namba za usajili T 312 AVG maeneo ya Kikatiti, Arumeru, Arusha.
 
Carista Charles Makoi enzi za uhai wake.
 Katika ajali hiyo, marehemu alifariki dunia papohapo huku wifi yake,  Jamhuri Makoi akifia Hospitali ya Rufaa ya KCMC, Moshi na mtoto wa marehemu, Brayan Makoi aliyekuwa amekaa siti ya nyuma akijeruhiwa vibaya. Hadi sasa amelazwa chumba cha uangalizi maalum (ICU) hospitalini hapo. 

Marehemu Carista ambaye siku ya tukio alivaa shati maafuru kwa jina la ‘makenzi’ rangi ya bluu na nyeupe, aliumia kichwani na kifuani na alibanwa na bodi ya gari kiasi kwamba, ili kuutoa mwili wake ilibidi wasamaria wema kutumia shoka kukata mabati sanjari na kuondoa paa la gari hilo. 

KAMANDA WA POLISI
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas alisema dereva wa basi bado anashikiliwa na polisi kwa uchunguzi zaidi.
Baadhi ya Wanafunzi 84 wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) wakiwa chini ya ulinzi kwa tuhuma za kuhamasisha uvunjifu wa amani Chuoni hapo na kufanya maandamano haramu kutoka Chuoni kuelekea katika Ofisi mbalimbali za viongozi wa Serikali zilizopo mjini Dodoma leo.
Baadhi ya Wanafunzi 84 wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) wakiwa kwenye gari ya polisi baada ya kutiwa mbaroni kwa tuhuma za kuhamasisha uvunjifu wa amani Chuoni hapo na kufanya maandamano haramu kutoka Chuoni kuelekea katika Ofisi mbalimbali za viongozi wa Serikali zilizopo mjini Dodoma leo.
 Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma inawashikilia wanafunzi 84 wa chuo Kikuu UDOM kwa tuhuma za kuhamasisha uvunjifu wa amani Chuoni na kufanya maandamano haramu kutoka Chuoni kuelekea katika Ofisi mbalimbali za viongozi wa Serikali zilizopo Dodoma Mjini leo tarehe 14.01.2015 majira ya 05:30hrs. 
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi DAVID MISIME – (SACP) ameeleza kuwa chanzo cha wananfunzi hao wa programu maalum ya Diploma ya Ualimu kufanya uhalifu huo ni kikao walichofanya wananfunzi hao tarehe 13.01.201 wakidai kuongezewa posho ya chakula na kwamba hata kiasi ambacho wanapewa wamechelewa kupewa. 

Hata hivyo uongozi wa Chuo uliwaeleza kuwa wenye mamlaka ya kuzungumzia swala la kuongezewa posho ni Bodi ya Mikopo na siyo chuo. Hivyo walitakiwa kufuata taratibu za kuwasilisha madai yao. Pia walielezwa kuwa hundi kwa ajili ya fedha za posho zao zimeshasainiwa na kuwasilishwa Benki ili waweze kuanza kupewa posho zao. 

Wanafunzi hao  hawakuridhika na usiku wakaanza kuhamasishana kufanya maandamano jambo ambalo ni kosa kisheria. Wanafunzi hao wamehojiwa kulingana na ushahidi ambao umekusanywa na wamefikishwa mahakamani kwa kosa la Kufanya Maandamano yasiyo na kibali. 

Viongozi waliohamasisha uvunjifu huo wa sheria baadi wamekamatwa na baadhi wanaendelea kutafutwa ili nao waweze kuchukuliwa hatua stahiki. Ushahidi uliokusanywa unaonyesha jinsi viongozi hao wameshiriki kuhamasisha kupitia vikao rasmi na visivyo rasmi, katika vikundi, kupita katika mabweni na kutuma sms. 

Kamanda MISIME ametoa wito kwa Wanafunzi hao kutumia taratibu zilizowekwa na Serikali na Chuo kuwasilisha malalamiko yao ngazi kwa ngazi na siyo kufanya vitendo vya kuvunja sheria ambavyo vitawasababishia kukamatwa. Endapo watafanya hivyo wasije kulaumu mtu kwani hatua zitachukuliwa kulingana na Sheria inavyoelekeza ikiwa ni pamoja na kufikishwa mahakamani.
Moja kati ya video zilizokua zinasubiriwa kwa hamu mithili ya video ya Mwana ya Alikiba ni hii ya Mwana FA "Kiboko Yangu" 

Mwana FA amesema katika video ambazo zime mgharimu ni hii hapa ya Kiboko yao,ambayoVideo hii ime imefanyiwa nchini Kenya na imeongozwa na director Kelvin Bosco Juniour wa Kenya!
Bonyeza Play hapa chini kuicheki video hiyo. Kama kifaa chako hakisomi player hii====>>BOFYA HAPA!

Design by GG greggy| Blogger Theme by greggy - Premium Blogger Templates | NewBloggerThemes.com