Thursday 20 November 2014



Mwanamke mmoja aliyejulikana kwa jina la Tatu Ikoko mkazi wa Mwananyamala jijini Dar, hivi karibuni alifunga mtaa kwa kutembea bila nguo baada ya kumfumania mumewe akiwa na mwanamke mwingine.
 Chanzo chetu cha kuaminika kilisema mwanamke huyo aliondoka nyumbani kwake usiku wa Ijumaa iliyopita na aliporejea asubuhi, alimkuta mwenzake akiwa na kigori mwingine ndani ndipo alipopagawa.
 
 


Tatu Ikoko akiwa katika hali ya kuvurugwa baada ya kumfuma mumewe na hawara.

“Alitoka usiku mzima akarudi saa moja asubuhi akamkuta bwana’ke yuko na mwanamke mwingine ndani,  akaanzisha vurugu, akavua nguo na kubaki na kanga moja na kuanza kupita mtaani huku akisema nivue nisivue na watu wakawa wanamuitikia vua.


 “Baada ya hapo tu watu wazima na mashosti zake  walimshika na kumsitiri, akaja bwana’ke akamchukua wakaenda nyumbani kwao,” kilisema chanzo hicho.


Chanzo kiliendelea kufunguka kuwa tukio hilo siyo mara ya kwanza kwa mwanamke huyo kwani alishawahi kufanya hivyo akiwa na mwanamume mwingine aliyejulikana kama Kisiso mtaani hapo na waliachana kwa tabia hiyo. 

 “Akiwa na mwanaume halafu akamfumania, ndiyo huwa anafanya hivi na yule mshikaji wa kwanza kwa aibu ilibidi ahame, sasa hivi anaishi Mbagala,” kilisema chanzo hicho.imeandikwa na shani ramadhani na mayasa mariwata.


Kenya Kimenuka kwa Wanawake Wanaovaa Nguo Fupi ama Suruali za Kubana na Kuachia Makalio , Mpaka sasa yameripotiwa matukio kadhaa ya wanawake waliovaa min Skirts  kushambuliwa na kuvuliwa nguo hadharani mbele za watu ..Hili Hapa chini ni tukio mojawapo …

 
As part of a social experiment by Model Prankster, model Leah Jung paraded around the streets of New York completely naked…with only a realistic-looking pair of jeans painted on her, complete with stitching and on-trend patches, making it look like she’s actually wearing jeans…but nobody even noticed she was naked.

The video, which was posted online last week has gone viral with millions of views. Model Praksters said did the experiment to determine how observant people of New York City are. They are apparently not very observant as 90% of the people who walked past Leah didn’t even notice she was naked. See the photos after the cut…


Basi la Sai Baba Express limepata ajali eneo la Pingo, Chalinze leo asubuhi baada ya kutaka kulipita basi lingine wakati mvua ikinyesha na kupelekea basi hilo kupinduka. Basi hilo lilikuwa linatokea Dar likielekea mkoani Mbeya. kwa taarifa za mapema zinasema kuwa akuna mtu aliyefariki katika ajali hiyo


Prizenta wa Kituo cha Radio E-FM cha jijini Dar, Penniel Mungilwa ‘VJ Penny’ anadaiwa kukumbwa na mauzauza yaliyodaiwa ni mapepo na kujikuta akipiga makelele barabarani.

Prizenta wa Kituo cha Radio E-FM cha jijini Dar, Penniel Mungilwa ‘VJ Penny’.
 Habari kutoka kwa shuhuda wetu zilidai kwamba, ishu hiyo ilijiri maeneo ya Makongo jijini Dar es Salaam, juzikati wakati staa huyo akielekea msibani ambapo rafiki yake kipenzi aitwaye Skitter alifariki dunia. 

Chanzo hicho kilidai kwamba Penny alikuwa akiendesha gari kwa mwendo wa kawaida, alipofika maeneo hayo aliegesha gari pembeni na kuanza kupiga kelele akilia kwa uchungu hivyo kuwaacha watu waliomshuhudia wakiwa midomo wazi wakitaka kujua kilichompata mtangazaji huyo. Mpashaji wetu huyo alizidi kueleza kwamba baada ya kama  dakika kumi, Penny aliondoa gari na kuendelea na safari. 

Paparazi wetu aliponyetishiwa ishu hiyo alimtafuta Penny na kumuuliza kuhusu tukio hilo ambapo alisema alikuwa akienda kwenye msiba wa rafiki yake, alipokaribia kufika alipata uchungu ndiyo akatokewa na hali hiyo.
Mwili wa marehemu aliyefahamika kwa jina moja la Betty baada ya kupigwa risasi leo asubuhi huko Yombo Vituka, Temeke jijini Dar es Salaam akiwa kwenye gari aina ya Toyota Pick Up mali ya Tunu Security na watu waliokuwa katika bodaboda.
Wananchi wakiwa eneo la tukio.
Mwili wa marehemu Betty ukibebwa na polisi kupelekwa Hospitali ya Chang'ombe, Dar kwa uchunguzi.
...Polisi wakiweka mwili wa marehemu ndani ya gari.
Mwili wa marehemu ukiwa ndani ya gari.
Mtu asiyefahamika (mwenye simu katikati) akiwasiliana na ndugu wa marehemu Betty baada ya kufika eneo la tukio.
DADA aliyefahamika kwa jina moja la Betty ameuawa kwa kupigwa risasi leo saa mbili asubuhi maeneo ya Yombo-Vituka, Temeke jijini Dar es Salaam akiwa kwenye gari aina ya Toyota Pick Up mali ya Tunu Security. 

Marehemu Betty ameuawa na watu waliokuwa kwenye bodaboda wakati akiwa kwenye gari la Tunu Security akitokea kituo cha mafuta kuelekea benki.

Watu hao waliokuwa kwenye bodaboda mmoja alimpiga dereva wa gari risasi ya mkononi alafu akampiga Betty risasi ya kichwani huku mlinzi aliyekuwa katika gari hilo akikimbia ambapo watu hao walichukua mfuko uliokuwa na pesa na kutokomea kusikojulikana.
Baadaye mwili wa marehemu ulichukuliwa na polisi na kupelekwa Hospitali ya Chang'ombe,Dar kwa ajili ya uchunguzi zaidi.
Design by GG greggy| Blogger Theme by greggy - Premium Blogger Templates | NewBloggerThemes.com