Tuesday 25 November 2014


Ni habari ya kusikitisha sana kupata taarifa hizi kwa kila mwenye moyo wa binadamu. Mtoto huyu ambaye alioneshwa akiteswa na house girl katika video iliyorekodiwa kwa siri na camera iliyotegeshwa sebuleni amefariki dunia. Mtoto alivunjika mbavu kutokana na kukanyagwa sehemu ya mbavu zake. Hivi leo tu tulipost video inaonesha jinsi ambayo mtoto huyu alikuwa akilazimishwa kula wakati akilishwa chakula kwa namna ya kikatili, na kishwa kupigwa na kukanyagwa mara tu alipotapika kutokana na kulishwa chakula kingi na kwa haraka. Hizi ni habari za kusikitisha sana mtoto mzuri kama huyu malaika asiye na makosa kukatizwa maisha yake kwenye mazingira kama haya. Mwandishi wetu anazidi kusisitiza juu ya umakini kwa wazazi na walezi wote kuwa makini katika kuwafahamu vizuri watu wanaowaachia watu wanaowaachia majukumu ya kuwalea watoto wao. Ni vyema kujipatia uhakika juu ya tabia za wasaidizi hawa wanaofanya kazi ya kushinda na kulea watoto wetu wakati wote ambao tunakuwa katika majukumu mengine ya kila ili kuweza kuendesha maisha yetu.


Ni kweli kwamba hatuwezi kufanya haya majukumu wenyewe bila usaidizi wa mabinti wa kazi. Wao ni muhimu na msaada mkubwa katika kuhakikisha kwamba watoto wanabaki salama na shughuli nyinginezo zinaendelea kama kawaida katika kuendesha maisha ya yetu na familia kwa ujumla. Lakini imetupasa kuwa makini kutokana na matukio kadhaa ya ukatili wa jinsi hii kwa watoto. Ni vyema kujua kwa undani tabia na mazingia ambayo msaidizi huyu amelelewa na kukua, na kupafahamu mahali anapotokea na ndugu zake.
Kama hukuona video ambayo ilikuwa ikionesha alichofanyiwa mtoto huyu ali mpaka anafariki dunia tazama hapa chini na uchukue hatua.








Kiungo wa Yanga, Haruna Niyonzima amezushiwa kifo na mtu asiyejulikana.
http://api.ning.com/files/EaBpbgf1JUZ1etoTyVZX2xQIO2eTwVtfoAulF*NcjqqL3yEGkMV49LM4Ii341ncUxbSOir1JlB3eIHHqyMIAufSSvuhakHt4/NIYONZIMA.jpg

Kiungo huyo mchezeshaji raia wa Rwanda, amezushiwa kuwa ameumia vibaya na baadaye kupoteza maisha katika ajali hiyo ya gari.

Habari hizo zimesambaa kwa kasi leo kuanzia alfajiri huku watu mbalimbali wakipiga simu kwenye blog hii na kuandika ujumbe wakitaka kujua nini tatizo.

Juhudi za kumpata Niyonzima zilifanyika na yeye akaeleza kuwa na taarifa hizo zilizomshangaza.

"Kwa kweli hata mimi imenishangaza, huyu mtu ambaye anaweza kuibuka na kusema maneno asiyoyajua.
"Niko nyumbani ninaumwa, sasa huyo mtu anayesema nimepata ajali ya gari wakati hata nyumbani sijatoka.

"Imenishangaza sana kwa kweli na hiki si kitu kizuri, ila ninamshukuru Mungu," alisema Niyonzima ambaye ni mtaratibu kitabia.
Credit. Salleh Jembe.com
Imetokea nchini India baada ya mama mmoja kujifungua mtoto mwenye miguu minne na mikono minne huku akipokelewa na wenyeji kwa furaha kubwa na kuitwa ‘Mungu Mvulana’
Mtoto huyo amepewa jina la ‘Mungu Mvulana‘ kwa kuwa kuzaliwa na viungo kama hivyo si jambo la kawaida na huchukuliwa kama mfano wa Mungu kwa jamii za kihindu na watu walisafiri kutoka kona mbalimbali za nchi hiyo  kwenda kumshuhudia mtoto huyo wa maajabu.

WAKATI TEAM WEMA WAKIENDELEA KUMPONDA ZARI KUWA NI MZEE NA ANA WATOTO! TEAM DIAMOND WACHARUKA KIIVI!

This is one of Diamond fan's INSTAGARM account....These are some of photos they posted....
Design by GG greggy| Blogger Theme by greggy - Premium Blogger Templates | NewBloggerThemes.com