Thursday 23 October 2014


Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Njombe, Fulgence Ngonyani akiangalia bweni la wanafunzi wa shule ya sekondari Njombe ambalo limeteketea kwa moto usiku

Kamishna wa Elimu Nchini Ameifunga Shule ya Sekondari ya Njombe (NJOSS) Kwa Muda wa Mwezi Mmoja Kutokana na Vurugu Zilizotokea Katika Shule Hiyo na Kusababisha Hasara ya Zaidi ya Shilingi Milioni Moja.
 Akifunga Shule Hiyo Kwa niaba ya Kamishna wa Elimu Nchini, Afisa Elimu Shule za Sekondari Mkoani Njombe Said Nyasiro Amesema Wameifunga Shule Hiyo Kutokana Uharibifu Uliofanywa na Wanafunzi Ikiwemo Kuchoma Jengo la Bweni na Karakana Pamoja Kupisha Uchunguzi Juu ya Tukio Hilo.

 Aidha Afisa Elimu Huyo Ameongeza Kuwa Kila Mwanafunzi Atatakiwa Kurejea Shuleni Hapo Akiwa na Mzazi Ama Mlezi Wake Pamoja na Shilingi Laki Moja na Elfu Hamsini Kwa Ajili ya Kufidia Mali Zilizoharibiwa .
 Akizungumzia Chanzo cha Tukio Hilo Mkuu wa Shule ya NJOSS Benard William Amesema Huenda Likahusishwa na Maamuzi ya Bodi ya Shule Hiyo Iliyokutana Oktoba 7 Mwaka Huu na Kuwasimamisha Masomo Wanafunzi Waliotoroka Nyakati za Usiku na Kwenda Kwenye Disko Katika Chuo cha Maendeleo Mjini NJombe, Huku Akisema Kuwa Uchunguzi Bado Unaendelea Kuhusiana na Tukio Hilo.

 Hata Hivyo Jeshi la Polisi Mkoa wa Njombe Linawashikilia Kwa Mahojiano ya Kina Baadhi ya Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Njombe NJOSS Wanaosadikiwa Kuhusika Katika Tukio Hilo.
 
Hata hivyo Baadhi ya Wanafunzi walionja Joto la Jiwe kutoka kwa polisi, Angalia picha zifuatazo.


 
Karibu upokee habari /picha Saa24 katika blog hii  Mchana /Usiku baada tu ya kujiunga kwa kubonyeza hapa>BONYEZA HAPA),Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp 0757929669





 




AKAUNTI ZAO FACEBOOK HIZI HAPA
Design by GG greggy| Blogger Theme by greggy - Premium Blogger Templates | NewBloggerThemes.com