Wednesday 22 October 2014

Week iliyopita Picha hiyo hapo juu ilienea mitandaoni ukimuonesha Freeman Mbowe na Mkewe Wakibusiana Live ....Mbowe Ameongea haya Kuhusu Picha hiyo :

“Kwanza mke wangu alikuwa anatimiza umri wa miaka 50 ya kuzaliwa, vilevile firstborn wetu Dudley alikuwa amemaliza shahada yake ya kwanza Chuo Kikuu cha Sussex, Uingereza, kwa mambo hayo mawili, tuliona ipo haja ya kufanya sherehe, ukizingatia watoto wetu wengine wawili Nicole na Denis walikuwa wamerejea nchini kwa sababu nao wanasoma nje ya nchi.

Siku hiyo ya tukio ilikuwa Jumapili, tulianza kwa kwenda kanisani Azania Front tukatoa sadaka, baada ya hapo tulikwenda Serena Hotel kwenye Ukumbi wa Kivukoni ambako chakula cha mchana kilikuwa kimeandaliwa, tukajumuika na ndugu wengine pamoja na marafiki.

“Haikuwa sherehe tu kusema labda nilikurupuka kumbusu mke wangu, ilikuwa sherehe ya kifamilia, kumpongeza mke wangu na mtoto wetu,” alisema Mbowe.

0 comments:

Post a Comment

Design by GG greggy| Blogger Theme by greggy - Premium Blogger Templates | NewBloggerThemes.com