Tuesday 7 October 2014

Spain 1Kuna Nesi mmoja amegudulika kuwa na ugonjwa wa Ebola baada ya kuwahudumia Wamishionari wawili waliokua na ugonjwa huo baada ya kutoka nao Sierra Leone walikokua wamekwenda kujitolea kufanya kazi.
Ugonjwa wa Ebola imekua ishu kubwa kwenye hizi nchi maarufu duniani ambazo zimejikuta zikiingia kwenye headlines baada ya Wagonjwa kuanza kugundulika ambapo Marekani kuna mmoja aliingia na Ebola kutokea Afrika na mwingine ni huyu Nesi wa Hispania.
Labda unaweza kushangaa ni jinsi gani huyu Nesi amekua akilindwa baada ya kujulikana amepata huo ugonjwa, hiyo picha ya juu sio msafara wa Kiongozi bali ni Polisi walikua wanamsindikiza Nesi huyo kumpeleka Hospitali ya Carlos III.
Hispania 2
Hawa ni Wafanyakazi nje ya hospitali ya La Paz University wakiwa wameungana pamoja kutoka Waziri wa Afya wa Hispania Ana Mato ajiuzulu baada ya mgonjwa wa Ebola kugundulika.
Baada ya kuugua Ebola Nesi huyu ambae bado jina lake wala sura yake havijaonyeshwa alisababisha Mume wake pamoja na watu wengine 50 kuwa chini ya uangalizi ili kujua kama na wao wameambukizwa lakini mpaka Jumanne jioni (October 7) hakuna yeyote kati yao aliekutwa na Ebola.
Kwenye sentensi nyingine ni kwamba Mwanaume wa Nigeria ambae aliingia Hispania siku kadhaa zilizopita pia alichukuliwa na kuchunguzwa lakini hakukutwa na Ebola, vivyo hivyo kwa Nesi mwingine ambae alikua akifanya kazi na Nesi wa kwanza aliekutwa na Ebola, baada ya kuharisha aliwekwa chini ya uchunguzi lakini ikagundulika hakuwa amepatwa na Ebola.
Unataka stori kama hizi zisikupite? unataka kuwa kupata kila kinachonifikia? karibu ujiunge na mimi kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Instagram Facebook



Mwanafunzi mmoja wa chuo kikuu maarufu nchini amejikuta akiumalizia  mwaka vibaya baada ya picha zake chafu kuvuja.... 

Katika picha hizo, mwanafunzi huyo anaonekana kujiachia uchi sakafuni huku wenzake wakimshangilia ndani ya chumba cha hosteli chao....

Picha si nzuri....una hiari ya kuziangalia au kutoziangalia. Kikubwa hapa kilikuwa ni kufikisha ujumbe kwa dada zetu ikiwa ni pamoja na kuwakumbusha thamani ya miili yao.

ANGALIA PICHA HAPA CHINI..



Kungu Masanja akiwa ndani ya gari la polisi


Wakazi wa kijiji cha Chibe kata ya Chibe katika manispaa ya Shinyanga wamepigwa butwaa baada ya mjumbe wa serikali ya kijiji hicho Kungu Masanja kukamatwa na askari polisi akiwa ameshikilia bango katika mbio za Mwenge wa Uhuru katika kijiji cha Chibe.

Kungu Masanja ambaye pia ni katibu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) katika kijiji cha Chibe alikutwa amebeba bango wakati kiongozi wa mbio za mwenge wa Uhuru mwaka huu Rachel Stephen Kassanda akifungua zahanati ya kijiji hicho.

Baadhi ya maneno yaliyokuwa yanasomeka katika bango hilo ni “KIONGOZI WA MBIO ZA MWENGE KITAIFA. 
I. HIVI MAPATO NA MATUMIZI YA ZAHANATI YA KIJIJI HUSOMWA WAPI?
II. HUJUI JENGO LA DAKTARI HARINA KIWANGO, KAMA HUJUI PITA NDANI YAKE.
III. KWA HOYO MACHACHE NITALALA TU POLISI.”

Muda mfupi baada ya kuonekana na bango hilo ghafla askari wa jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga walimkamata na kuondoka naye huku wakazi wa eneo hilo wakibaki midomo wazi.

Akizungumza akiwa chini ya ulinzi wa askari polisi Masanja alidai kuwa aliyoyaandika yako sahihi na kwamba hajashawishiwa na mtu yeyote ameamua kuandika ujumbe ili ufanyiwe kazi.

Akizungumza na Malunde1 blog diwani wa kata hiyo Mahona Gwisu Kameja kupitia Chama Cha Mapinduzi alisema alishangaa kumwona kijana huyo akiwa ndani ya gari la polisi.

“Binafsi sikuona bango hilo, wala sikumwona wakati anakamatwa, hilo jengo analodai liko chini ya kiwango lilijengwa mwaka 2009 kwa nguvu ya wananchi, serikali na TASAF likigharimu shilingi milioni 52 Tangu mwezi Septemba 2014 linatumiwa na mganga na wauguzi wa zahanati iliyozinduliwa leo,” alisema Diwani huyo.

“Hata hivyo mimi nashangaa huyu kijana ni mjumbe wa serikali ya kijiji. Kama limejengwa chini ya kiwango basi yeye anapaswa kuwajibika, haiwezekani mjumbe wa kijiji ajikaange mwenyewe. Hapa kuna UCHADEMA maana huyu ni kiongozi wa CHADEMA katika kijiji hiki. Labda katumwa,” aliongeza diwani Kameja.

Naye mkurugenzi wa manispaa ya Shinyanga Festo Kang’ombe aliiambia Malunde1 blog kuwa jengo hilo limejengwa katika kiwango kinachotakiwa ndiyo maana linatumika hivi sasa.

Kwa upande wake kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru 2014 Rachel Stephen Kassanda alisema jengo lililotengenezewa bango siyo lile la zahanati waliyoifungua hivyo hawezi kulizungumzia.

Kassanda alisema mamlaka/majukumu aliyopewa katika mbio za mwenge ni kuzungumzia miradi iliyoko kwenye ratiba aliyopangiwa hivyo suala hilo wanaohusika ni halmashauri husika.

Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga Justus Kamugisha alipotafutwa na mwandishi wa habari hizi kuzungumzia kuhusu kukamatwa kwa kijana huyo alisema yuko nje ya ofisi, ingawa hata kaimu kamanda wa polisi Longinus Tibishishubwa alipopigiwa simu zaidi ya mara moja haikupokelewa siku hiyo.


Kungu Masanja akiwa ndani ya gari la polisi muda mfupi baada ya kuonekana na bango kwenye mbio za Mwenge wa Uhuru kaitka Kata ya Chibe, Manispaa ya Shinyanga
Design by GG greggy| Blogger Theme by greggy - Premium Blogger Templates | NewBloggerThemes.com