Saturday 17 January 2015

News II

Mwanamke mmoja Hawa Kundani akiwa ameongozana na mtangazaji Joyce Kiria, amezua taharuki kwenye kikao cha Kamati ya Bunge ya Katiba, Sheria na Utawala, baada ya kuvamia na kulalamika kwamba ametelekezwa na mumewe ambaye ni Mbunge wa Dimani Zanzibar, Abdallah Sharia Ameir wakati huo walikuwa wakijadiliana suala la Mahakama ya Kadhi, kikao kilichokuwa kikifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere.
Mwanamke huyo alidai kuwa wana watoto wengine wawili aliozaa na Mbunge huyo, mkubwa ana miaka tisa na mwingine miaka sita ambao walichukuliwa na mumewe huyo akawapeleka kulelewa na mwanamke aliyemuoa.
Kwa upande wa mbunge hiyo Ameir alidai kwamba kesi yao ipo kwenye Mahakama ya Kadhi, akidai kwamba mwanamke huyo amekuwa akimdhalilisha kwa kupitia mtoto huyo mlemavu ambaye alikiri ni mwanaye.
Akizungumzia tukio hilo Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Gosbert Blandes alisema ni tukio ambalo limewafedhehesha kwa kuwa hawakulitarajia. 
MWANANCHI
Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), imeiagiza Bodi ya Sukari Tanzania (SBT) kumwondoa katika nyumba ya bodi hiyo, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Mahusiano na Uratibu), Stephen Wasira kutokana na kuishi katika nyumba hiyo kinyume na taratibu ambapo alianza kuishi kwenye nyumba hiyo akiwa Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika.
Mkurugenzi Mtendaji wa SBT, Henry Semwaza aliieleza Kamati ya PAC kuwa wamekuwa wakifanya jitihada za kuwasiliana na Wasira kuhusu kuirejesha nyumba hiyo, lakini hakuna utekelezaji wowote unaofanyika.
Mwenyekiti wa PAC, Zitto Kabwe akitoa azimio la Kamati hiyo alisema, “Hapa hakuna msukumo mnaoufanya yaani tangu mwaka 2012 mlipomwandikia barua mpaka sasa kimya. Tunaiagiza SBT kumwandikia barua Wasira mkimtaka arejeshe nyumba na nakala ya barua hiyo tuipate Jumatatu.”
Zitto pia alimwagiza Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika, Sophia Kaduma amwandikie barua Katibu Mkuu Kiongozi kuhusu uamuzi huo wa Kamati.
MTANZANIA
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Magesa Mulongo amebuni aina mpya ya ulinzi wake binafsi pamoja na msafara wa magari unaoambatana naye anapokuwa katika ziara zake, msafara wake unafanana na ule wa viongozi wakuu wa kitaifa, Rais na Waziri Mkuu,
Msafara huo hujumuisha askari wa usalama barabarani ambao kazi yao ni kujipanga barabarani ili kuzuia magari mengine ili msafara wake upite, pia huambatana na Mkuu wa Polisi wa wilaya husika, maofisa usalama wa wilaya na mkoa, watumishi wa Halmashauri ya Jiji na maofisa wa wilaya anazozitembelea.
Sambamba na msafara huo wa magari, Mulongo pia analindwa na makundi matatu ya wanausalama ambao ni askari polisi wa kawaida, askari kanzu na maofisa usalama wa taifa.
Ingawa amekuwa akitumia aina hii ya ulinzi na usafiri hata katika safari zake za kawaida asubuhi anapotoka katika hoteli ya kitalii anayoishi kwenda ofisini wake, katika ziara yake ya kujitambulisha kwa wakazi wa Mkoa wa Mwanza aliyoianzia Wilaya ya Ilemela, ulinzi wake ulionekana kuimarishwa zaidi, huku idadi ya magari kwenye msafara wake nayo ikiongezeka.
Watu waliozungumza na Mtanzania kuhusu msafara huo kushangazwa na kusema msafara wa aina hiyo una chembechembe za vitisho pamoja na kugharimu kiasi kikubwa cha fedha.
NIPASHE
Vita ya ubunge baina  Mbunge wa Same Mashariki (CCM), Anne Kilango Malecela na Mkuu wa Wilaya ya Mbozi (DC)   Dk. Michael Kadeghe, imezidi kufukuta Kilango akitishia kumshitaki kwenye  Sekretarieti ya Baraza la Maadili ya Viongozi wa Umma, kwa kupeperusha bendera ya taifa kwenye gari lake akiwa  wilayani Same huku akijua ni kosa.
Kadeghe anadaiwa kuanza ‘kucheza rafu’ za uchaguzi mkuu ujao kwa kutishia harakati za Kilango kutetea kiti chake jimboni humo kwa kupita na gari lake lenye namba STK 3764 aina ya Land Cruiser huku akipeperusha bendera ya taifa.
Mkuu huyo wa Wilaya alidaiwa kuendesha vikao vya ndani vya siri vya Chama cha Mapinduzi (CCM) kabla ya wakati kwa nia ya kutaka kumng’oa ubunge Kilango.
Nitakutana na Mwenyekiti wa Sekretarieti ya Baraza la Maadili ya Viongozi wa Umma ili kutafuta haki. Haiwezekani wewe siyo DC wa Same upeperushe bendera kwenye eneo ambalo huliongozi?”—Anne Kilango Malecela.
Dk. Kadeghe alipinga kufanya vikao vya siri vya chama kwa ajili ya kuendesha kampeni ya kumng’oa kwenye ubunge, kuhusu ishu ya bendera amesema kuwa ilikuwa ikifanyiwa usafi na wala haikuwa inapepea kama ambavyo inadaiwa.
Katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2005, Kilango alimshinda Dk. Kadeghe kwa kura 389 dhidi ya kura 46 alizoambulia kwenye uchaguzi ndani wa CCM na mwaka 2010, Kilangopia  alimshinda kwenye kura za maoni kwa kupata kura 7,900 dhidi ya kura 2,200 alizoambulia Kadeghe.
HABARI LEO
Wakazi wa Nzega, Tabora wamewapiga, kuwaua na kuwachoma moto watu watatu kwa tuhuma za kushiriki kumuua Helena Abel na kumjeruhi mume wake, Said Msoma.
Kamanda wa Polisi Tabora, Juma Bwile amethibitisha kuokea kwa tukio hilo ambapo Helena Abel na mume wake Said Msoma walivamiwa katika tukio hilo, Helena aliuawa na Said Msoma alifanikiwa kumjeruhi mmoja wa wahalifu hao ambaye alikimbia.
Kamanda Juma amesema wananchi walifanya doria na kumkamata mhalifu huyo aliyejeruhiwa ambaye anaitwa Mainda Mahila na kuanza kumhoji kuhusika na mauaji hayo na kukiri kufanya hivyo.
Bwile alisema kuwa mtuhumiwa huyo aliwaeleza wananchi hao kuwa mauaji hayo alifanya kwa kuagizwa na Mama Zainabu Hamis pamoja na mtoto wake, Zena Yasoda ambapo wananchi hao waliwapata watuhumiwa wote wawili kisha kuanza kuwapiga hadi kufa na baadaye kuwachoma moto.
Wakati huohuo mtu mmoja Chenge Kasinki alivamiwa na kuuawa nyumbani kwake na watu wasiofahamika
 Ni halali yako kupata kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonye
Ongwen kulia
Mwendesha mashtaka nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati anasema kuwa kamanda wa cheo cha juu wa kundi la Lord's Resistance Army LRA nchini Uganda amekabidhiwa wawakilishi wa mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita ICC.
Mwendesha mashtaka huyo alisema kuwa Dominic Ongwen anayeshutumiwa kwa kuendesha uhalifu dhidi ya binadamu atasafirishwa kwenda mjini Hague hii leo.
Ongwen alichukuliwa kama mwanajeshi mtoto na kundi la LRA kabla ya kukamatwa na wanajeshi wa Marekani wiki iliyopita.
Design by GG greggy| Blogger Theme by greggy - Premium Blogger Templates | NewBloggerThemes.com