Sunday, 19 October 2014



Ange Kagame hivi karibuni amekuwa gumzo kwenye mitandao ya kijamii na kuzidi kujiongezea umaarufu, hii sio tu kwasababu ni mtoto wa pili na wakike pekee kati ya watoto wanne wa raisi Kagame bali muonekano wake wenye mvuto asilia umefanya wengine kufikia hatua ya kumfananisha na Cleopatra.

Ange alizaliwa mwaka 1989 na kwa mda mrefu amekuwa kwenye masomo nje ya nchi hivyo hajapata kufahamika sana mpaka hivi karibuni alipo msindikiza baba yake raisi Kagame kwenye hafla ya jioni iliyo wakutanisha viongozi wa Afrika huko Marekani.

Picha zake zimepata kuzagaa kwenye mitandao ya kijamii na wengi wamesifia uzuri wake na kuweka picha zake alizo piga kwenye matukio mbalimbali kwenye mitandao yao. ungana na ngastuka.com ili uweze kumfahamu zaidi Ange kwa jicho la tatu, yani tuangalie maisha yake kwa ujumla na mchango wake katika jamii kama kijana wa kiafrika.





Kwa mujibu wa IGIHE, Ange ni msichana mwenye msimamo na kutegemea mazuri siku zote, mtu anaye tekwa na hisia kali lakini pia ni msichana mtiifu na muaminifu, huku wenzake  walio soma nae wakimsifia kuwa ana akili sana darasani.

Ange hupendelea zaidi kula vyakula tofauti tofauti, kutembelea migahawa mbalimbali hasa ile mipya na kusafiri. Kwenye  michezo ana penda zaidi  mpira wa kikapu na hushabikia Boston Celtics timu inayo shiriki ligi ya kikapu ya NBA Marekani.




Kitendo cha hivi majuzi cha kumsindikiza baba yake kwenye hafla ya jioni iliyofanyika ikulu ya Marekani kimehusishwa na jambo la kisiasa lakini yeye mwenyewe kwenye ukurasa wake wa Twitter ameshangazwa na hilo jambo na kukanusha skendo hiyo nakusema “huwa mnakaribia lakini mnashindwa kugusa ukweli wa mambo”

Ukitazamia ukurasa  wake wa Twitter, Ange ameonekana kuwa ni msichana anaye pendelea zaidi muziki michezo na burudani. Hata hivyo, amekuwa akishea nyimbo anazo zipenda zaidi kwa marafiki na kipindi cha Kombe la dunia amekuwa akizipongeza timu za Afrika kwa uwezo walio onesha, hii inaashiria kuwa sio mtu anaye zipa uzito habari za siasa labda kwa huko mbeleni.

Ange amekuwa pia akishiriki kwenye matukio ya uchangiaji huko Kigali akisaidia shughuli za maendelea,utoaji chanjo, elimu pamoja na kuwainua wanawake huku akifwata nyayo  za mama yake Jeanette Kagame ambaye ni mwenyekiti wa mfuko wa Imbuto (Imbuto Foundation).
Kwa sasa Ange yupo mwaka wa mwisho wamasoma yake ya Chuo kikuu.
- See more at: http://www.ngastuka.com/2014/08/mjue-kiundani-ange-wa-kagame.html#sthash.gvXs66L4.dpuf

0 comments:

Post a Comment

Design by GG greggy| Blogger Theme by greggy - Premium Blogger Templates | NewBloggerThemes.com