Monday, 6 October 2014

Tumekwisha! Kikosi maalum cha Oparesheni Fichua Maovu (OFM) cha Global Publishers, kimemnasa msaidizi wa kazi za ndani (hausigeli) akifanya biashara haramu ya kuuza mwili kwa kisingizio cha mshahara kiduchu.

Kushoto ni hausigeli akifanya biashara ya uchangudoa maeneo ya Sinza jijini Dar.
Tukio hilo la aina yake liliingia kwenye kamera za OFM maeneo ya Sinza jijini Dar, mwishoni mwa wiki iliyopita ambapo msichana huyo wa kazi alikutwa kwenye harakati za kusaka wanaume ili kuwapa penzi kwa malipo.
Mara baada ya kumnasa na kumlamba picha akiwa na wenzake ambao nao kama yeye walikuwa wamevaa nguo fupi yaani nusu utupu, alianza kuangua kilio hasa alipokuwa akihojiwa kwa nini anajihusisha na biashara hiyo hatarishi katika maisha yake.
“Jamani mmenipiga picha  mtanipotezea kazi yangu, jamani mimi nimeajiriwa, ni mfanyakazi wa ndani kwa mheshimiwa Mikocheni (Dar), nafanya kazi za ndani hii yote ni kujitafutia riziki nje ya kazi,” alilalama binti huyo aliyekadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 20 hadi 23.
Baadhi ya machangudoa wakiwa mawindoni.
Binti huyo aliwaambia OFM kwamba alifikia hatua hiyo ya kujiingiza katika biashara hiyo ya ngono kutokana na ugumu wa maisha huku lawama akizielekeza kwenye mshahara kidogo wa kazi za ndani.
“Mshahara wangu ni mdogo sana, nalipwa shilingi elfu 50 kwa mwezi, nina watoto wawili kijijini hivyo hautoshi. Kama vipi nitafutieni kazi nitaacha kuuza mwili,” alisema.
Alipoulizwa namna anavyotoka kwa bosi wake kwenda kujiuza, hausigeli huyo alisema kwamba huwa anakula dili na walinzi wa bosi wake usiku wakiwa wamelala anatoka na akirudi freshi anawakatia walinzi chao.
Ads by SenseAd Options
Ads by SenseAd Options
Machangudoa wengine wakizikimbia kamera za Global.
Alisema kuwa yeye analala katika vyumba vya uani kwa hiyo anapotoka waajiri wake hao inakuwa vigumu kumsikia kwani wanakuwa wamepitiwa na usingizi.
Aliendelea kueleza kwamba kuna siku nyingine huwa anarudi nyumbani akiwa amevuna fedha nyingi kuliko mshahara wake.
“Hii kazi yangu inaniingizia kipato kikubwa sana kuliko mshahara,” alisema hausigeli huyo

0 comments:

Post a Comment

Design by GG greggy| Blogger Theme by greggy - Premium Blogger Templates | NewBloggerThemes.com