WAKATI mabinti wengi hasa mastaa wa Bongo wakijuta baada ya picha zao za utupu walizopigwa na wapenzi wao kuvuja, kwa msanii mrembo aliyepambavideo ya wimbo wa Bongo Fleva uitwao Jambojambo wa msanii Steve R&B, Aisha Firozi ‘Sapna’ ni kawaida kwani hujifotoa mwenyewe.


Ukistaajabu ya Musa utayaona ya Firauni; Sapna alipopigiwa simu na paparazi wetu na kuelezwa kuhusu kunaswa kwa picha hizo, kwanza alishangaa lakini akakiri kuzitambua.
“Hizo kweli ni picha zangu na nilijipiga mwenyewe sasa sijui wewe umezipataje na zimefi kaje huko kwenu? Mimi nilipiga kwa masilahi yangu mwenyewe, huwa natamani sana kujiangalia jinsi umbo langu lilivyo, ndiyo maana niliamua kujipiga na si vinginevyo.
“Kila mtu na maisha yake na mimi sikuwa na dhamira mbaya kujipiga picha hizo zaidi ya kujiangalia tu nilivyo,” alisema Sapna.
0 comments:
Post a Comment