Saturday 18 October 2014


Mwimbaji maarufu Davido kutoka Nigeria tayari ametua Dar es Salaam Alhamisi usiku akitokea kwao Nigeria ambapo dakika 20 baada ya kutua alikubali kukaa na kuongea mawili matatu yawafikie Watanzania.

Moja kati ya vitu alivyoongea ni kuhusu album yake mpya itayotoka mwanzoni mwa mwaka ujao lakini pia kuna mastaa wawili wa dunia ambao amewashirikisha kwenye nyimbo mbili za hiyo album, hayuko tayari kuwataja kwa sasa.

Utampata Davido mwenyewe katika mapoz zake on The Truth: Davido Wednesday, 22 October saa 21:00 CAT katika MTV Base.

Kingine ni kwamba Mafikizolo, Uhuru na Diamond Platnumz wa Tanzania ni miongoni mwa mastaa wa Afrika ambao sauti zao zitasikika kwenye hiyo album.

Kuna swali aliulizwa kuhusu kumjua msanii yeyote wa Tanzania zaidi ya Diamond. Alichojibu ni: "Sitodanganya. Kiukweli simfahamu yeyote zaidi ya Diamond."

Namalizia na hii nukuu: “Nilikosa tuzo yoyote mwaka 2013 na ilinikasirisha sana ila sikukubali kukata tamaa sababu nimekosa tuzo, sikutaka initawale kwamba mimi sio mkali, niliamua kuondoa kichwani kwangu kwamba tuzo sio ishu kubwa ukikosa.”

Usikose kumtazama Davido katika The Truth: Davido Wednesday, 22 October saa 21:00 CAT katika MTV Base.

0 comments:

Post a Comment

Design by GG greggy| Blogger Theme by greggy - Premium Blogger Templates | NewBloggerThemes.com