Thursday, 18 December 2014

Wanajeshi wa jehsi la Nigeria
Mhakama moja ya kijeshi nchini Nigeria imewahukumu kifo askari 54 kwa kukataa kupigana na kundi la wapiganaji wa Kiislamu la Boko Haram.
Wanajeshi hao ambao walipatikana na kosa la uasi,walituhumiwa kukataa kuikomboa miji mitatu iliyokuwa imetekwa na Boko Haram mwezi Agosti.
Wakili wa wanajeshi hao 54 alisema kuwa watawauwa kwa kupigwa risasi huku wengine watano wakiachiliwa huru.
Wanajeshi wamelalamika kuwa hawapewi silaha na mabomu ya kutosha kupigana na Boko Harm.
Kundi hilo limekuwa likipigana tangu mwaka 2009 na linalenga kujenga nchi inayoongozwa na sheria za Kiislamu kaskazini mashariki mwa Nigeria.
Zaidi ya watu 2000 wameuwawa katika mashambulizi yaliyolaumiwa kufanywa na kundi hilo kufikia sasa mwaka huu na maelfu zaidi ya watu wamelazimishwa kuhama makwao kutokana na vita vinavyoendelea.
Koti hiyo ya kijeshi ilianza mwezi Oktoba na ilifanywa kwa siri.Viongozi wa kijeshi hawakupatikana kuzungumzia swala hilo.
Wakili anayewawakilisha,Femi Falana,alisema kuwa wanajeshi hao wote walituhumiwa ''kupanga njama ya kuasi dhidi ya mamlaka ya kikosi cha Divisheni ya 7 cha jeshi ya Nigeria.''
Wanajeshi wote walikataa mashtaka na hukumu hiyo inasubiri idhini ya maafisa wa ngazi za juu.
Katika kisa sawia mwezi Septemba,wanajeshi 12 walihukumiwa kifo kwa makosa ya uasi na jaribio la kumuua afisa wa jeshi katika mji wa kaskazini-mashariki wa Maiduguri.

0 comments:

Post a Comment

Design by GG greggy| Blogger Theme by greggy - Premium Blogger Templates | NewBloggerThemes.com