5. World One
Jengo hili linatarajiwa kuwa refu kuliko yote Duniania ambayo yamejengwa kwa ajili ya makazi ya watu. World One ipo mjini Mumbai nchini India ambapo matajiri wanatarajiwa kuishi mahali hapo kwa kodi ya dola milioni 1.5 nyumba ya vumba vitatu mpaka vinne. Pamoja na hayo jingo hili litakuwa refu kuliko yote mjini Mumbai ambapo litakuwa na ghorofa 117. Ujenzi wa ghorofa hii unatarajiwa kukamilika 2015
4. Agora Garden Tower
Ni majengo mawili pacha yaliyoshikana,uejenzi wake utakamilika 2016 jijini Taipei nchini Taiwan. Utofauti wake ni kwamba kila sehem ambayo ghorofa inaunganika kutakuwa na bustani za mboga mboga, miti ya matunda na bustani za kupumzika.
3. The Dubai Pearl
Hii ni sehem ya starehe Duniani ambapo wageni wengi toka mabara tofauti husussani Ulaya hufika na kupumzika nchini hapo. Dubai Pearl imezungukwa na maduka mengi ya vitu mbalimbali ambapo ni minara mine ya ghorofa tofauti zilizounganishwa kwa juu. Jengo hili liliaza kujengwa mwaka 2009 na litakamilika 2016 ambapo tamasha la maadhimisho ya filamu kimataifa yatakuwa yakifanyika hapo.
2. Shanghai Tower
Jengo hili liliaza kujengwa 1993 nchini China ambapo lipo katika matengenezo ya mwisho kabla ya kuzinduliwa rasmi 2015. Shanghai Tower ina ghorofa 121 na limeigharimu China kiasi cha dola bilioni 4.2.
1. Kingdom Tower
Jengo hili limeaza kujengwa 2013 mji wa Jeddah nchini Saudi Arabia na linatarajiwa kukamilika 2019. Kingdom Tower lintarajiwa kuwa jingo refu kupita yote Duniani kwa kuwa na ghororfa 157. Ujenzi wa jingo hilo la kisasa unatarajiwa kugharimu dola bilioni 1.2. Ndani ya jingo hili kutakuwa na nyumba za kuishi, ofisi mbalimbali, hoteli kubwa nne za kisasa, pamoja na kituo cha uchunguzi.
0 comments:
Post a Comment