Monday 3 November 2014



Jaji Joseph Warioba akitoa mada.

Mtoa mada katika mdahalo wa kujadili Katiba inayopendekezwa, Jaji Joseph Warioba akitoa mada kabla 
ya mkutano huo kuvunjika katika ukumbi wa Ubungo Plaza jijini Dar es Saam leo.

Baadhi ya vijana walioingia na mabango ndani ya ukumbi wa mkutano wakiwa na mabango yaliyokuwa 
yakisomeka ‘Katiba inayopendekezwa tumeipokea tunaiunga mkono’.

Mlinzi wa Jaji Joseph Warioba (kushoto) akimkinga kwa mikono ili asipate madhara baada ya mdahalo wa 
kujadili Katiba inayopendekezwa kuvamiwa na kundi la vijana na kusababisha uvunjifu wa amani. 

Jaji Joseph Warioba akiangalia usalama wake kabla ya kuondolewa mlinzi wake katika ukumbi wa Ubungo Plaza 
ambapo mdahalo wa kuijadili Katiba inayopendekezwa ulikuwa ukifanyika kabla ya kuvunjika.

Aliyekuwa mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Humphrey Polepole akimzuia mmoja wa vijana aliyekuwa
 na jazba mara baada ya kutokea kwa vurugu katika mdahalo wa kujadili Katiba inayopendekeza.

Mkurugenzi wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere (MNF), Joseph Butiku (katikati) akisindikizwa kuingia katika chumba cha VIP mara
 baada ya kuvunjika kwa mdahalo wa kujadili Katiba inayopendekezwa. Mdahalo huo uliandalia na taasisi hiyo.



 Vijana wakiwa na mabango.
Fujo zinaanza.


Baadhi ya viti vilivyovujwa.

Jaji Mstaafu Mh. Joseph Sinde Warioba akisaidiwa kuondolewa kwenye
 Mdahalo huo mara baada ya kuzuka kwa tafrani hiyo.

Jaji Mstaafu Mh. Joseph Sinde Warioba akisaidiwa na wanausalama wa kuondolewa
 kwenye mdahalo huo mara baada ya mambo kuharibika kutokana na vurugu kubwa.





Jaji Warioba akitoka katika ukumbi huku akisindikizwa na askari kanzu.

 Jaji Warioba akiwapungia mkono wananchi waliokuwa wamefurika nje ya jengo la Ubungo Plaza
 ambako mdahalo wa kujadili Katiba inayopendekezwa ulikuwa ukifanyika.

Wananchi walikuwa nje ya jengo la Ubungo Plaza wakimshangilia Jaji Warioba wakati akitoka katika
 ukumbi wa mdahalo huku wakimuita 'Rais Rais'. 

0 comments:

Post a Comment

Design by GG greggy| Blogger Theme by greggy - Premium Blogger Templates | NewBloggerThemes.com