Sunday 12 October 2014


Written By Jo Cyberspace on Sunday, 28 September 2014 | 18:17



Mlima Ontake. 

Takriban wakwea milima 30 huenda wameaga dunia nchini Japan kufuatia kulipuka kwa mlima wa Volcano siku ya Jumamosi na kusababisha kukwama kwa mamia ya raia hao karibu na kilele cha mlima huo.

Makundi ya uokoaji yanasema kuwa yalipata miili karibu na kilele cha mlima Ontake. 

Wakwea milima katika mlima Ontake
Waokoaji hao wamefanikiwa kufika kwenye kilele cha mlima huo ambapo ndege ya kijeshi aina ya helikopta ilitumiwa kuwaokoa karibu watu 40 waliokuwa wamejeruhiwa.


Zaidi ya wakwea milima 200 walifanikiwa kuteremka kutoka kwa mlima huo wenye urefu wa mita 3000 wakati mlima huo ulipoanza kutupa mawe na majivu bila ya kutoa onyo lolote.
Baadhi yao walisema kuwa walishindwa kupumua kutokana na majivu yaliyokuwa yakianguka kutoka angani.

0 comments:

Post a Comment

Design by GG greggy| Blogger Theme by greggy - Premium Blogger Templates | NewBloggerThemes.com