Sunday 12 October 2014


Askari wa jiji wakiwapakia wafanyabiashara kwenye ‘Karandinga’ ya askari polisi.
Baada ya kupigwa  mabomu ya machozi.
Wananchi wakikimbia.
Mwenye mkoba haya, mwenye mtoto twende…!!
Jamaa akifuta machozi.
Mama mwenye mtoto akinawa maji usoni, pembeni vijana wakinawishana.
Vuta nikuvute ya kutafuta maji ya kunawa.
Gari la polisi likielekea eneo la tukio kuongeza nguvu.
ASKARI wa jiji jana walilazimika kutumia mabomu ya  machozi kuwatawanya watu wanaofanya biashara kandokando mwa barabara ‘Machinga’ katika maeneo ya Tabata jijini Dar es Salaam.
Mmoja wa wakazi wa eneo hilo, aliyezungumza na GPL, alifafanua chanzo cha askari kutumia nguvu hiyo, ambapo alisema ni baada ya wananchi kuwapiga mawe wakati wakitekeleza zoezi lao. 

“Majuzi  askari wa jiji walikwenda maeneo ya Segerea kwa ajili ya kufanya oparesheni ya kuwaondoa wafanya biashara kandokando mwa barabara, wananchi wakaanza kuwapiga mawe na kufanya zoezi hilo kuwa gumu. Ndiyo maana leo baada ya kuanza kupigwa mawe, nao wakaamua kutumia mabomu ya machozi katika kuwatawanya.’’

0 comments:

Post a Comment

Design by GG greggy| Blogger Theme by greggy - Premium Blogger Templates | NewBloggerThemes.com