Sunday 19 October 2014

libya
Marekani na mataiafa manne ya bara Ulaya yamelaani ghasia zinazoendelea nchini Libya na kutaka mapigano hayo kusitishwa mara moja.
Libya imeshuhudia mapigano siku za hivi karibuni kati ya makundi hasimu yaliyoibuka wakati wa vita vya kumuondoa madarakani aliyekuwa kiongozi wa nchi hiyo Muammar Gaddafi.
Kwenye taarifa ya pamoja Ufaransa, Ujerumani , Uingereza , Italia na Marekani wanasema kuwa uhuru uliopatikana kwa njia ngumu nchini Libya uko hatarini iwapo makundi ya kigaidi nchini Libya na kutoka nje yataruhusiwa kutumia nchi hiyo kama maficho salama.
Taarifa kutoka nchi hizo inasema kuwa changamoto za kisiasa zitatatuliwa tu ikiwa kutakuwa na jeshi linaloongozwa na serikali iliyochaguliwa kidemokrasia.

0 comments:

Post a Comment

Design by GG greggy| Blogger Theme by greggy - Premium Blogger Templates | NewBloggerThemes.com