Saturday, 13 September 2014


BOFYA HAPO CHINI KUANGALIA HIZO PICHA,ANGALIZO KAMA WEWE NI MTOTO USIBOFYE PICHA PITA PEMBENI





You might also like:
Baba mmoja aliyetambulika kwa jina moja la Kaga mkazi wa Mwanga Kisangani ''B'' jirani na Saigoni amemuua mpenzi wake kwa kumnyonga na kumtumpa katika makorongo ya Kilimahewa ''B'' Chini ya Shule ya Msingi Kilimahewa.

Taarifa za awali zinasema kulikuwa na ugomvi baina yao hao wapenzi wawili hali iliyopelekea mwanamke (Mama Koku) kumshtaki mwanaume mahakamani na kusababisha Mwanaume kufungwa miezi miwili jela. 
 
Siku kadhaaa baada ya mwanaume kutoka gerezani alipata habari kuwa mpenzi wake huyo aliyesababisha kuwekwa ndani anatembea na mwanaume mwingine ndipo mwanaume huyo alipopanga njama/namna ya kutekeleza mauwaji hayo.

Taarifa zinasema mara baada ya mwanaume kudhamiria kutekeleza tukio hilo lililo kinyume na neno la MUNGU katika kitabu kile cha Kutoka 20.13 alimwambia mpenzi wake kuwa; "Leo nimejisikia tutoke out twende Beach za Gorden tukajivinjari"  Mwanamke (Mama Koku) bila shaka lolote aliongozana nae mpenzi wake huyo ndipo wakiwa njiani katika makorongo ya Kilimahewa ''B'' mwanaume alimbadilikia ghafla na kumkaba kooni mwanamke na kupelekea kupoteza maisha. 

Mara baada ya mwaume kufanya unyama huo inasemekana zilipita siku kadhaa ndipo mwanaume alipowapiga simu kwa ndugu wa mwanamke huyo; "Njooni mchukue mzoga wenu!" Aliongea mwanaume huyo.
Mwanaume huyo anajishughulisha na shughuli za ubebaji mizigo katika soko kuu la Kigoma Mjini. 

Mara baada ya mwanaume huyo muuwaji kutoa taarifa kwa ndugu wa marehemu,ndugu walifanya jitihada za kumtafuta ndugu yao ndipo walipoukuta mwili katika Makorongo ya Kilimahewa ukiwa umeharibika vibaya na walilazimika kuzika hapo hapo.

Jeshi la Polis mkoani Kigoma linaendelea kumtafuta mtuhumiwa na atakapopatikana atapelekwa katika vyombo vya sheria.

Taarifa hii imethibitishwa na Diwani wa kata ya Mwanga Kaskazini Mh.Fransic Mangapi. 

MFANYABIASHARA maarufu nchini Nigeria amefariki dunia mara baada ya kubakwa na wake zake watano kati ya sita anaowamiliki. Hiyo ni kwa mujibu wa gazeti la Dail Mail. Awali Kabla ya kurejea nyumbani kwake inatajwa kuwa Uroko Onoja alikuwa akipata ulabu wake (pombe) katika baa moja huko Ugbugbu katika jiji la Benue hadi mida ya majogoo.

Tajiri huyo mfanyabiashara aliporejea nyumbani kwake huku akiwa na usongo wa mambo nyeti ya sita kwa sita, aliamua kukata kiu kwa mke wake mdogo (mke wa sita). Hata hivyo, wake zake wakubwa watano ile kuona hatua hiyo, ndipo walipoingiwa na wivu nao wakachukuwa hatua ya kutinga chumbani nao wapewe mambo. Wakiwa na silaha za asili kama visu na fimbo walivamia kitanda cha Onoja na kumlazimisha to have sex with them as well.

Wednesday, 10 September 2014

Nyuma ya tukio la denti wa darasa la tano kwenye shule moja ya msingi iliyopo Mbezi-Shamba, Dar, aliyejitambulisha kwa jina moja la Irene (11) la kunaswa akifanya utapeli kwa kuwaibia raia, mazito yameibuka.

Denti wa darasa la tano anayetambulika kwa jina moja la Irene (11) aliyenaswa akiwatapeli raia.
 Katika tukio hilo lililojiri hivi karibuni maeneo ya Posta Mpya, Dar, denti huyo alikuwa akisimama nyakati za asubuhi akivalia sare za shule huku akiombaomba kwa madai kuwa hana nauli ya kuvukia katika kivuko cha Kigamboni kwenda shule anayosoma. 

Kwa mujibu wa mmoja wa mashuhuda, mtoto huyo alikuwa akisimama mbele  ya Kituo cha Daladala cha Posta mpya akijifanya ombaomba kwa madai kwamba hana  nauli.Ilisemekana kwamba siku nyingine mtoto huyo alikuwa akionekana akiuza simu kwa bei chee na alipohojiwa alikokuwa akizitoa alidai ameziokota.
Mwandishi  Gabriel Ng'osha (kushoto) akipata undani wa habari katika tukio hilo. 
 Dereva mmoja, Juma Hamis anayeegesha gari lake eneo hilo (Posta Mpya) alisema kuwa tabia ya mtoto huyo ilikuwa ni ya muda mrefu kwani alianzia Kariakoo, Dar akitapeli na kuiba madukani ambapo watu walimstukia hivyo akaamua kuhamia Posta. 

“Mara kadhaa amenusurika kupigwa akidaiwa kuchomoa simu za watu kwenye mikoba ndani ya daladala.“Kukamatwa kwa Irene, watu wa maofisini na kwenye daladala wameshukuru kwani anafahamika na ni tishio kwa utapeli na ndiyo waliomchoma kwa polisi akadakwa baada ya kukutwa akijidai ni ombaomba,” alisema dereva huyo.
Ofisa wa Polisi kutoka 'Central Police' Posta akifafanua jambo kuhusiana na mkasa huo.
 Jader Sapi, anayefanya kazi katika ofisi moja zilizo ndani ya jengo la IPS, alisema mtoto huyo aliwahi kuingia ofisini kwao na alipotoka, wafanyakazi wawili walilalamika kupotea kwa simu zao, kitu kilichowafanya wajue ni yeye. 

Mama mmoja aliyeshuhudia Irene akichukuliwa na askari, alisema ameshawahi kumpa fedha mara kadhaa denti huyo, akiamini alivyomweleza kuwa hakuna na wazazi na hivyo hana nauli ya kumpeleka shuleni. 
Akizungumza na gazeti hili akiwa mikononi mwa polisi kwenye Kituo Kikuu, Irene alisema ni mwanafunzi wa shule moja ya msingi (jina kapuni) iliyopo Mbezi-Shamba na siyo kama alivyokuwa akidanganya kuwa anasoma Kigamboni, Dar.
Wananchi wakishuhudia laivu tukio hilo lililotokea maeneo ya Posta mpya, Dar es Salaam.
 Pia alikiri kwamba amekuwa akidanganya kuwa hana wazazi wakati ukweli ni kwamba wazazi wake wapo.“Ni shetani tu aliniingia nikawadanganya raia,’’ alisema Irene. 

Baada ya kushuhudia tukio hilo, wanahabari wetu walimsaka mkuu wa shule anayosoma mtoto huyo, Yusuph Zenny ambaye alikiri kumfahamu Irene na kudai kuwa tayari taarifa kutoka Kituo Kikuu cha Polisi, Dar zilimfikia. 

Alitobosa siri kuwa ameshapata malalamiko mara kadhaa kuhusiana na binti huyo na kwamba amekuwa akifanya uchunguzi ili kupata ukweli. 

Hata hivyo, alisema anawasiliana na wazazi ili kulifuatilia sakata hilo hivyo kuwaomba wanahabari wetu wampe muda atatoa majibu au hatua itakayochukuliwahuku Irene akiwa bado mikononi mwa polisi kwenye dawati la jinsia.
Toa maoni yako hapo chini tafadhali...!

Monday, 8 September 2014


  Babu Seya na× Kocha wakiwa nje ya mahakama.
Ads by OnlineBrowserAdvertisingAd Options

MAISHA ya uraiani baada ya kutoka gerezani ndiyo mzozo uliopo sasa kati ya wanamuziki mahiri nchini ambao ni baba na mwana, Nguza Vicking ‘Babu Seya’ na Johnson Nguza ‘Papii Kocha’, Amani limetonywa.
 

Chanzo makini kimesema kuwa wawili hao wamefikia hali hiyo baada ya kila mmoja kuanika dira ya maisha yake ya uraiani baada ya kuachiwa kutoka katika kutumikia kifungo cha maisha jela katika× Gereza la Ukonga.





“Ishu kubwa ni maisha ya uraiani,× Papii amemhakikishia baba yake kwamba akiwa uraiani ataendelea na muziki jambo ambalo×Seya hakubaliani nalo hata kidogo,” kilisema chanzo cha ndani. 



Kikaendelea: “Unajua yule mzee (Babu Seya) yeye anaamini kwamba uraiani lazima wabadili staili ya maisha kwa vile kuwa kwao huru kuna mkono wa× Mungu kwa hiyo kuendelea kuishi maisha ya kidunia ni kutorudisha shukurani kwake.”



 
Nguza Viking ‘Babu Seya’ (wa pili kulia) na mwanaye Johnson Nguza ‘Papii Kocha’ (wa pili kushoto) wakiwa mahakamani.

MSIMAMO WA BABU SEYA 

Wakati Papii Kocha akianika msimamo huo kwa baba yake ambao ulisababisha wazozane, mzee huyo yeye ameweka wazi kwamba maisha yake ya uraiani ni ya kumtumikia× Mungu mwanzo mwisho.



“Lakini Babu Seya alimlaumu sana mwanaye kwamba kuendelea kufanya mambo ya duniani ni kutomtendea haki× Mungu kwa vile nguvu zake ndiyo mwanga wa maisha yao mapya,” kilisema chanzo. 
 



HAYA YOTE YAMEKUJAJE?

Chanzo kilisema mambo hayo yote yameibuka kufuatia rufaa zote za wafungwa hao kupigwa chini na hivyo hatima yao kuwa mikononi mwa× Rais wa Jamhuri ya× Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ‘JK’ ambapo wanaamini wapo huru tayari kinachosubiriwa ni siku tu.
 



Chanzo: “Unajua imani ni kitu cha ajabu sana. Yeye (Babu Seya) anachoamini wapo huru tayari, ila siku ndiyo ya kuvutia subira lakini pia anaamini mbali na msamaha wa JK, Mungu anatenda.” 



BABU SEYA ATATUA KANISA LA LIFE IN CHRIST





 

 
Babu Seya na× Kocha wakiwa nje ya mahakama.

NGUZA MBANGU AONGEA NA AMANI

Baada ya taarifa zote hizo, juzi× Amani lilimtafuta Nguza Mbangu ili kumsikia alichonacho kuhusu maisha ya baba yake uraiani, hasa suala la kuokoka na kumrudia Mungu.
 



Mbangu: “Suala la kuokoka ni la× Mungu mwenyewe akiamua kumvuta mtu. Kama nia ya moyo wake ni hiyo basi ina maana mzee (baba) ameshavutwa. 



“Kwanza nataka nikwambie kitu× Ndauka, siku zile baba na× Papii waliposhindwa rufaa magazeti yaliandika sana, ooooh! Babu Seya na mwanaye kufia jela. Mimi nakwambia hivi, suala la baba na Johnson (Papii) watu wamekuwa wakiliangalia kimwili. 



“Mimi ninachojua wale wapo huru hata leo hii (juzi Jumanne), nilishakwambia siku za nyuma na leo narudia tena,× Tanzaniaitamshangaa sana Mungu kupitia wale watu (Babu Seya na Papii).



“Tena nakuahidi kwamba, siku si nyingi, pengine mwezi huuhuu. Yaani, sijui nikwambiaje, nitakupigia simu, nadhani keshokutwa (leo Alhamisi), ndipo utajua nilikuwa namaanisha nini,” alisema× Mbangu kwa kujiamini. 
 



TUREJEE NYUMA 

Juni 25, 2004, Babu Seya, Papii Kocha, Nguza Mbangu na× Nguza walihukumiwa kifungo cha maisha jela baada ya kupatikana na hatia ya ubakaji na kuwanajisi watoto 8 wa× Shule ya Msingi, Mashujaa, Sinza jijini× Dar. Hukumu hiyo ilitolewa katika× Mahakamaya Hakimu Mkazi ya× Kisutu chini ya Hakimu Eddy Lyamuya. Walikata rufaa Mahakama Kuu. 
 



Januari 27, 2005 rufaa yao ya kwanza ilisikilizwa ambapo Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, Thomas Mihayo aliitupilia mbali. 



Februari 10, 2010 Mahakama ya Rufaa ilikazia hukumu ya Kisutu kwa Babu Seya na Papii Kocha, lakini ikawaachia huru watoto wengine wawili wa mwanamuziki huyo, Nguza Mbangu na Francis Nguza
Design by GG greggy| Blogger Theme by greggy - Premium Blogger Templates | NewBloggerThemes.com