Tuesday 25 November 2014






Kiungo wa Yanga, Haruna Niyonzima amezushiwa kifo na mtu asiyejulikana.
http://api.ning.com/files/EaBpbgf1JUZ1etoTyVZX2xQIO2eTwVtfoAulF*NcjqqL3yEGkMV49LM4Ii341ncUxbSOir1JlB3eIHHqyMIAufSSvuhakHt4/NIYONZIMA.jpg

Kiungo huyo mchezeshaji raia wa Rwanda, amezushiwa kuwa ameumia vibaya na baadaye kupoteza maisha katika ajali hiyo ya gari.

Habari hizo zimesambaa kwa kasi leo kuanzia alfajiri huku watu mbalimbali wakipiga simu kwenye blog hii na kuandika ujumbe wakitaka kujua nini tatizo.

Juhudi za kumpata Niyonzima zilifanyika na yeye akaeleza kuwa na taarifa hizo zilizomshangaza.

"Kwa kweli hata mimi imenishangaza, huyu mtu ambaye anaweza kuibuka na kusema maneno asiyoyajua.
"Niko nyumbani ninaumwa, sasa huyo mtu anayesema nimepata ajali ya gari wakati hata nyumbani sijatoka.

"Imenishangaza sana kwa kweli na hiki si kitu kizuri, ila ninamshukuru Mungu," alisema Niyonzima ambaye ni mtaratibu kitabia.
Credit. Salleh Jembe.com

0 comments:

Post a Comment

Design by GG greggy| Blogger Theme by greggy - Premium Blogger Templates | NewBloggerThemes.com