Thursday 4 December 2014

Misiba ya vijana wawili,Matei John Mmassy Mfanyabiashara na mmiliki wa Klabu maarufu mjini Dodoma ya Matei Lounge na Wakili wa kujitegemea na Mkufunzi wa Chuo Kikuu cha St. John, Joseph Joshua Oguda waliofariki kwa ajali ya gari maeneo ya Ranchi ya mifugo,Narco iliyopo Kongwa nje kidogo ya mji wa Dodoma mapema wiki hii wakitokea Mjini Morogoro vimetikisa mji wa Dodoma na Viunga vyake.

Miili ya marehemu hao imeagwa leo kuanzia mchana katika ibada ya pamoja iliyo fanyika katika Uwanja wa Nyerere Squire mjiji Dodoma.Miili yote imesafirishwa jioni hii wakati Mwili wa Marehemu Matei umepelekwa Mkoani Kilimanjaro na Mwili wa Marehemu Joshua Ogunda umepelekwa Musoma,Mkoani Mara kwa ajili ya tararibu za Mazishi.

Majeneza yenye miili ya marehemu Joshua na Matei wakati wa ibada maalum ya kuwaombea iliyofanyika kwenye Uwanja wa Nyerere mjini Dodoma

Sehemu ya Umati wa waombolezaji wa Misiba hiyo.


Waombolezaji wa wakiwa kwenye foleni ya kwenda kuaga miili ya Marehemu hao.

0 comments:

Post a Comment

Design by GG greggy| Blogger Theme by greggy - Premium Blogger Templates | NewBloggerThemes.com