Monday 6 October 2014

Jeshi la wananchi wa Tanzania JWTZ limelaani vikali askari wake kikosi cha kiteule cha nyandoto 27 KJ makoko ambaye anadaiwa kushindwa kutii maelekezo ya askari polisi wa Usalama Barabarani wilayani Tarime na kusabisha fujo na vurugu kubwa huku polisi wakitumia risasi za moto kudhibiti hali hiyo.Akitoa tamko hilo jeshi la wananchi wa Tanzania mbele ya waandishi wa habari mjini Musoma, mkuu wa Brigedi 202 kundi la vikosi kanda ya magharibi Brigedia jenerali Mathiew Mayela sukambi amesema kwa niaba ya mkuu wa majeshi nchini, kitendo hicho cha aibu kimefanywa na askari binafsi na siyo Jeshi la wananchi na kwamba askari huyo amekiuka kiapo chake hivyo hastahili kuendelea kuitwa mwanajeshi wa Jeshi hilo. 
Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) limelaani kitendo cha askari wake wa kikosi cha Nyandoto 27 KJ Makoko ambaye inadaiwa alishindwa kutii maelekezo ya askari polisi wa Usalama Barabarani wilayani Tarime, Mara na kusabisha mapigano baina ya wanajeshi na polisi.
Katika tukio hilo ambalo lilitokea Oktoba Mosi, mwaka huu jioni katika kituo cha mabasi mjini Tarime, raia mmoja na askari kadhaa wa Jeshi la Polisi wakiongozwa na Mkuu wa Upelekezi wa Makosa ya Jinai (RCO) Kanda maalum ya Tarime /Rorya na askari wawili wa JWTZ walijeruhiwa kwa risasi.

Mkuu wa Brigedi 202 kundi la vikosi kanda ya Magharibi, Brigedia Jenerali Mathew Mayela Sukambi, akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Majeshi, alisema kitendo hicho cha aibu kimefanywa na askari binafsi na siyo JWTZ.

Alisema askari huyo amekiuka kiapo chake, hivyo hastahili kuendelea kuitwa mwanajeshi wa jeshi hilo na kwamba ameagiza sheria na taratibu zichukuliwe dhidi yake pamoja na wote walioshiriki katika tukio hilo.

“Kitendo hicho kimefanywa na askari binafsi na siyo jeshi, taratibu za jeshi zinafundisha na kueleza afisa na askari kuwa mtiifu na mwenye nidhamu na kutakiwa kutii mamlaka na kufuata sheria za nchi kwa mujibu wa katiba,” ilieleza sehemu ya tamko hilo la JWTZ. 

Alisema kuwa chanzo cha fujo na vurugu hizo zilisabishwa na askari wa Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani kumkamata askari wa JWTZ kwa kosa la kuendesha pikipiki bila kuvaa kofia ngumu (Helment) na baada ya majibishano askari huyo aliita wenzake walikuwa jirani kwa ajili ya msaada ndipo polisi waliitana kwa wingi na kuanza kutumia nguvu kwa kutumia risasi za moto kuzima vurugu hizo.

Aliwataka maofisa na askari wa jeshi hilo kuzingatia viapo vyao, kutii sheria na taratibu za nchi, mamlaka ya kiraia kwa mujibu wa katiba ya Tanzania huku akiwaonya raia kuacha kushabikia matukio mabaya pindi yanapotokea. 

kuhusu Migogoro ya mipaka kati ya wananchi na vikosi vya Jeshi,mkuu huyo wa Brigedi 202 kundi la vikosi kanda ya magharibi Brigedia jenerali sukambi,amewaonya baadhi ya watu wasipeonda kuheshimu mipaka ya vikosi vya jeshi.

Aidha kiongozi huyo wa Jeshi la wananchi wa tanzania kanda ya magharibi,ametumia nafasi hiyo kuwataka wanasiasa kuacha mara moja kuingiza masuala ya siasa ndani katika utendaji wa mambo ya kijeshi. 

Katika tukio hilo ambalo lilitokea oktoba mosi mwaka huu majira ya saa kumi na moja jioni eneo la kituo cha mabasi mjini tarime, raia mmoja na askari kadhaa wa jeshi la polisi wakiongozwa na mkuu wa upelekezi wa makosa ya jinai (RCO) kanda maalum ya Tarime Rorya pamoja na askari wawili wa Jeshi la wananchi walijeruhiwa kwa risasri wakati wa kuzima vurugu hizo.
- See more at: http://wajanjawatowns.blogspot.com/2014/10/jwtz-walaani-askari-wake-kuwa-chanzo.html#sthash.0NtemlXK.dpuf

0 comments:

Post a Comment

Design by GG greggy| Blogger Theme by greggy - Premium Blogger Templates | NewBloggerThemes.com